NA MWANDISHI WETU
CHAMA Cha Soka Mkoa wa Pwani, COREFA, Agosti 27 mwaka huu kinaratajia kufanya uzinduzi wa kituo kingine cha michezo wilayani Mkuranga mkoani humo ikiwa ni muendelezo wa mikakati ya Mwenyekiti, Robert Munisi, wa kuhakikisha kwamba kila Wilaya inakuwa na vituo hivyo.
Kituo hicho cha pili, kitazinduliwa katika Shule ya Msingi Mkuranga kuanzia saa tano asubuhi na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya, Hadija Nasiri Ally.
COREFA, inakwenda kuzindua kituo hicho cha pili ambapo awali kituo cha kwanza kilizinduliwa Agosti 20 mwaka huu na Katibu Tawala, Mosses Magogwa, katika Uwanja wa Bwawani Kibaha mkoani Pwani na jumla ya vijana zaidi ya 600 wenye umri wa miaka 15, 17 na 20 walisajiliwa katika kituo hicho.
“ Tunakwenda kuweka rekodi nyingine ndani ya Wilaya ya Mkuranga, lengo ni kuhakikisha kwamba mpira mkoa wa pwani unachezwa, kituo hiki kitakuwa na manufaa kwa vijana wanaopenda mpira kutimiza ndoto zao, ni zamu ya watu wa Mkuranga kunufaika na COREFA ambayo inataka kufanya mambo makubwa katika mpira wetu ndani ya Mkoa wa Pwani.
Aidha jambo hili ni kubwa, na ni heshima kwa watu wa Mkuranga hivyo, nitoe wito siku ya Jumapili kujitokeza kwa wingi kwa lengo la kufanikisha uzinduzi huo wa kituo cha michezo kwa vijana wetu kwani wote tunafahamu kuwa mpira ni ajira.
No comments:
Post a Comment