WAZIRI MKUU MSTAAFU PINDA APATA ELIMU YA HALI YA HEWA, ATEMBELEA BANDA LA TMA MAONESHO YA NANENANE - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Monday, August 7, 2023

WAZIRI MKUU MSTAAFU PINDA APATA ELIMU YA HALI YA HEWA, ATEMBELEA BANDA LA TMA MAONESHO YA NANENANE

 


NA MWANDISHI WETU, MBEYA

WAZIRI Mkuu Mtaafu wa Awamu ya nne, Mizengo Pinda ametembelea banda la Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) lililopo katika viwanja vya John Mwakangale, Uyole mkoani Mbeya, kupitia Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea kufanyika kuanzia tangu tarehe 01 hadi 08 Agosti 2023.

 Pinda akiwa ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Charles Makongoro Nyerere pamoja na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa, Gerald Kusaya, amepata elimu ya hali ya hewa kutoka kwa Meneja wa Huduma za Hali ya Hewa Kilimo, Isack Yonah na kujionea namna kifaa chenye Teknolojia ya kisasa kinavyopima taarifa mbalimbali za hali ya hewa.

Aidha, kupitia maonesho hayo, wadau pamoja na wanafunzi mbalimbali wameendelea kumiminika katika banda hilo ili kujifunza na kupata ufafanuzi wa taarifa mbalimbali zinazotolewa na TMA.

 


No comments:

Post a Comment