BASHUNGWA AWASILI WILAYANI MAFIA KWA ZIARA YA KIKAZI. - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, March 22, 2024

BASHUNGWA AWASILI WILAYANI MAFIA KWA ZIARA YA KIKAZI.


WAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa (Mb) amewasili wilayani Mafia mkoani Pwani kufanya ziara ya kikazi  ambapo amepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Aziza Mangosongo, leo Machi 22, 2024.


Bashungwa amepokelewa pia na Mbunge wa Mafia ambaye pia ni Naibu Waziri wa Elimu, Omary Kipanga pamoja na viongozi wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi.


Katika ziara hiyo, Waziri Bashungwa atakagua miundombinu ya barabara ikiwa ni pamoja na Barabara ya Kilindoni - Kigamboni, barabara ya Kilindoni - Utende, Kivuko cha Kilindoni pamoja na kufanya mkutano wa hadhara Kirongwe.

No comments:

Post a Comment