KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UWEKEZAJI WA MITAJI YA UMMA (PIC) YARIDHISHWA NA MRADI WA UMEME - MTWARA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, March 26, 2024

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UWEKEZAJI WA MITAJI YA UMMA (PIC) YARIDHISHWA NA MRADI WA UMEME - MTWARA


NA MWANDISHI WETU, MTWARA

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma(PIC) imeridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa mradi wa kuzalisha Umeme kwa njia ya gesi asilia uliopo  kitongoji cha Hiari Mkoani Mtwara.


Akizungumza Machi 25, 2024 kwenye ziara ya Kamati  katika kituo hicho ,Mwenyekiti wa kamati, Deus Sangu amesema kuwa Kamati imeridhishwa na uwekezaji uliofanyika katika mradi huo  na kuwa Serikali imewekeza  kiasi cha Shilingi Bilioni 3.6 ili kukamilisha ujenzi wa mradi 


“kwa kipindi cha  miezi 12 iliyopita kulikua kuna kelele nyingi za Umeme katika Maeneo ya Lindi na Mtwara, lakini Mhe.Raisi alitoa kiasi cha shilingi Bilioni 3.6 ili kutekeleza ujenzi wa mradi huu ambao utazalisha kiasi cha Megawati 20 na hivyo kumaliza kabisa changamoto ya Umeme katika Mikoa ya Lindi na Mtwara”Alisema Sangu


Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya PIC Augustine Vuma ,ameishukuru Serikali na kusema kuwa kuwa kamati imeridhishwa na uwekezaji mkubwa uliofanyika katika mradi huo 


“ kwaniaba ya Kamati kwanza  nimpongeze Rais wetu,Dkt.Samiah suluhu Hassan, Wizara yenyewe kupitia Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt.Dotto Biteko na TANESCO kwa ujumla, kwa tumia resource walizonazo kwa maana ya mitambo na fedha kidogo kutatua changamoto ya Umeme katika mikoa ya Lindi na Mtwara, sisi kama kamati tumeridhishwa na uwekezaji huu” alisema Vuma


Aidha ametoa rai kwa wananchi wa Lindi na Mtwara kutumia umeme kama fursa ya kiuchumi katika kujiongezea kipato na maendeleo


Akizungumza kwa Niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi TANESCO, Mjumbe wa Bodi  Mha.Isaac Chanji, ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha zilizowezesha ujenzi wa mradi na pia amewapongeza wafanyakazi wa TANESCO kwa kukamilisha kazi kwa wakati na ndani ya Bajeti


“Kwa Niaba ya Mwenyekiti wa Bodi kipekee tunaishukuru Serikali, na hasa Raisi wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuipa kipaumbele Miradi ya Nishati na kutoa fedha kiasi cha Bilioni 3.6 kwaajili ya kukamilisha Mradi huu, na kama Bodi tumefurahishwa na kazi kubwa iliyofanyika mahali hapa, kwanza kwa kuwekwa huu mtambo ambao utasaidia kuimarisha hali ya upatikanaji wa Umeme hapa Mtwara, 

Pia tunawapongeza wafanyakazi wa TANESCO pamoja na Mkandarasi kwa kukamilisha kazi hii kwa wakati, ndani ya miezi mitatu tu kama walivyoahidi “ alisema Chanji


Naye Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO ,Mha.Gissima Nyamohanga amesema kuwa kazi ya kusimika Mtambo katika mradi huo imekamilika na hivyo umeme utaanza kuzalishwa katika eneo hili


“Nimpongeze Raisi wetu,Dkt.Samiah Suluhu Hassan kwa kuwezesha mradi huu, aliona fursa katika mkoa wa Lindi na Mtwara kama Mikoa inayochangia katika pato la uchumi wa Taifa na hivyo uwepo wa umeme wa kutosha katika mikoa hii kutatoa fursa ya wawekezaji kuwekeza ,na hivyo kuongeza uchumi wa wakazi wa Lindi na Mtwara na Taifa kwa ujumla.






No comments:

Post a Comment