Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Habari kuhusu mafanikio ya miaka mitatu ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Machi 24, 2024 jijini Dar es Salaam
NA MAGENDELA HAMISI
TANZANIA katika kipindi Cha miaka mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, yangu aingie madarakani imefanikiwa kuwa na akiba ya kutosha ya fedha za kigeni ambapo kwa sasa zimefikia dola za Marekani bilioni 5.4.
"Tunashukuru Kwa Sasa akiba ya fedha za kigeni imeendelea kuwa toshelezi katika kipindi chote cha miaka mitatu hadi Desemba 2023, taifa limekua na akiba inayotosha kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi kwa miezi 4.5, ikiwa ni kiwango cha juu ya lengo la miezi 4, akiba hiyo ni sawa na dola za Marekani bilioni 5.4”
Hayo yamesemwa Leo na Msemaji wa Serikali, Mobhare Matinyi, wakati akizungumza na waandishi na wahariri wa vyombo vya habari nchini na kufafanua kuwa Tanzania imeendelea kuwa kwenye kundi la nchi zenye uchumi wa pato la kati, ikimaanisha pato la wastani la kila mwanachi kwa mwaka (GNI per capital) ambapo ingawa mwaka 2019 ilikuwa kiasi cha dola 1,080 (Tsh. 2,743,813) lakini mwaka 2022 ni dola 1,200 ( Tsh. 3,048,681).
Ameongeza kuwa licha ya uchumi wa Tanzania kuendelea kukua, ulitetereka wakati wa mlipuko wa UVIKO-19 na uwepo vita za Urusi na Ukraine na Mashariki ya Kati, ambapo kabla ya changamoto hizo ulifikia ukuaji wa uchumia asilimia 7 na baadae ukashuka na kufika asilimia 4.2 kwa 2020 na sasa umepanda na kufikia asilimia 5.2
“Serikali pia imeendelea kudhibiti mfumuko wa bei ambapo kwa sasa ni chini ya 4% - kiwango ambacho ni miongoni mwa viwango bora katika nchi za jumuiya za kikanda ambazo Tanzania ni mwanachama, kama Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), amesema.
.jpg)




No comments:
Post a Comment