NA MWANDISHI WETU, KENYA
TANZANIA na Kenya zimekubaliana na kutia saini makubaliano ya
kuondoa vikwazo vya kibiashara visivyo vya kiushuru ili kuruhusu raia kutoka
nchi hizo kufanya biashara baina yao kwa urahisi na kwa manufaa ya pande zote
mbili.
Makubaliano hayo yametiwa saini na Wakili Stephen Byabato Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiwa na mwenzake
Mhe. Rebbecca Miano, Waziri wa Uwekezaji, Biashara na Viwanda kutoka nchini
Kenya. Makubaliano hayo yamefikiwa wakati wa Mkutano wa nane (8) wa Kamati ya
Pamoja ya Biashara baina ya Tanzania na Kenya katika ngazi ya Mawaziri uliofanyika
Kisumu nchini Kenya Machi 22, 2024.
Mkutano huo ulianza kwa ngazi ya watalaam kisha ngazi ya Makatibu
Wakuu ambapo zaidi ya vikwazo vya kibiashara visivyo vya kiushuru zaidi ya 14
vilijadiliwa na kuwekewa mpango wa kuendelea kuviondoa vyote.
Tanzania na Kenya ni wabia wakubwa wa biashara na hivyo kuondolewa
kwa vikwazo hivyo vitasaidia kuongezeka mara dufu kiwango cha kufanyika kwa
biashara baina ya mataifa hayo.









No comments:
Post a Comment