Mkuu wa Wilaya ya Masasi Lauteri Kanoni, akifungua kikao cha wadau na wateja wa Bohari ya Dawa (MSD), Kanda ya Mtwara Machi 22, 2024.
...........................
NA MWANDISHI WETU, MTWARA
WADAU wa Afya wa Bohari ya
Dawa (MSD) Kanda ya Mtwara wamehimizwa kusimamia matumizi sahihi ya
takwimu za mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya, ili ziwawezeshe kufanya maamuzi
sahihi juu ya bidhaa hizo katika maeneo yao.
Akifungua kikao cha wadau
na wateja wa MSD kanda ya Mtwara, Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Lauteri Kanoni
amesema uwepo wa takwimu sahihi unaiwezesha MSD kuagiza kwa usahihi bidhaa za
afya na kuboresha upatikanaji wa bidhaa hizo kwenye vituo vya kutolea huduma za
afya.
Aidha, amewashauri MSD
kuhakikisha utaratibu wa vikao vya mwaka vya wadau ni muhimu kwa pande
zote mbili, yaani Bohari ya Dawa (MSD) yenyewe na wadau ili kwa pamoja
kuboresha upatikanaji wa bidhaa za afya, kwa kujadili changamoto na kuzitafutia
utatuzi.
Kwa upande wake Meneja wa
MSD Kanda ya Mtwara Tea Malay ameeleza kuwa kwa sasa kanda ya MSD Mtwara
inahudumia vituo vya kutolea huduma za afya 631, na inasambaza bidhaa za afya
kila baada miezi miwili.
Naye Meneja Huduma kwa Wateja na Miradi Dkt. Pamella Sawa ameeleza kuwa vikao vya MSD na wadau wake kuanzia sasa vitakuwa endelevu kila mwaka.
Meneja wa MSD Kanda ya Mtwara Tea Malay, akizungumza kwenye kikao hicho








No comments:
Post a Comment