HAMADI RASHID ANG’ATUKA, APIGIWA CHAPUO KUWANIA URAIS, AINYOOSHEA KIDOLE TUME HURU YA UCHAGUZI ZANZIBAR - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, May 29, 2024

HAMADI RASHID ANG’ATUKA, APIGIWA CHAPUO KUWANIA URAIS, AINYOOSHEA KIDOLE TUME HURU YA UCHAGUZI ZANZIBAR


 NA MAGENDELA HAMISI

MWENYEKITI wa Chama Cha Alliance For Democratic Change (ADC), Hamad Rashid ameng’atuka katika nafasi hivyo baada ya kuitumikia kwa kipindi cha miaka 10 na anapigiwa chapuo kuchukua fomu ya kunai urais, Zanzibar kwa ajili ya kuipeperusha bendera ya chama hicho katika uchuguzi mkuu ujao 2025.

Wakati akitangaza kung’atuka katika nafasi hiyo leo, Mei 29, 2024 jijini Dar es Salaam, pia ametangaza rasmi kuwa Juni 27 mwaka huu uchaguzi mkuu wa chama hicho utafanyika ili kuziba nafasi za juu kwa ajili ya kuiongoza ADC katika kipindi kingine cha miaka mitano.

“Chama chetu kimetimiza miaka zaidi ya miaka 10 na katiba yetu inatuelekeza kufanya kushiriki chaguzi za ndani ya chama na nje na hakuna tunazozisusia, mkiona hatushiriki basi sababu kubwa ni changamoto ya kifedha.

“Katiba yetu imetuelekeza kufanya uchaguzi kila miaka mitano, Mwenyekiti, Katibu wakifanikiwa kutimiza miaka 10 wanapaswa kuachia ngazi ili nafasi hizo zichukuliwe na wengine kwa kufanya uchaguzi, hivyo naondoka katika nafasi hiyo kikatiba ingawa hainizuii kugombea nafasi nyingine ikiwemo urais na si ubunge au uwakilishi kwani huko nimeshatoka,” amesema.

Amesema kuwa ikiwa wajumbe wataridhia anaweza kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu ujao kwa ajili ya kuipeperusha bendera ya chama hicho visiwani Zanzibar jambo ambalo liliungwa mkono na Katibu MKuu wa Chama hicho,” Hassan Doyo.

“Kazi kubwa ya kutukuka umeifanya katika kipindi cha miaka 10, ikiwemo kukiongoza chama katika kipindi chote kikiwa hakina fedha za uhakika jambo ambalo ilikuwa ni kazi kubwa na leo umekifikisha cha katika uchaguzi baada ya miaka 10 kwa kweli tunakushukuru sana.

“Kila chama kina utaratibu wake na umesema afya yako bado ni imara na tunamshukuru Mungu kwa hilo na wenzetu wa vyama vingine wanasema kuwa fomu ya urais hakuna wa kuichukua, nasi ADC tunasema kwa demokrasia hiyo hiyo, Zanzibar hakuna wa kuchukua fomu ya urais zaidi ya Hamad Rashid ingawa hatuzuii, mwanachama mwingine kuchukua fomu hiyo,” amesema Doyo.

Hamad Rashid wakati akimalizia hotuba yake ya kung’atika katika nafasi ya uenyekiti alitoa wito kwa wanachama kujitokeza kuchukua fomu kuwania nafasi za juu ya chama na kusisitiza tume itakayoundwa kusimamia uchaguzi itakuwa huru na itatenda haki kuwa wanahofu ya Mungu katika kutimiza majukumu yao.

“Nafasi hii sasa iko wazi na ningependa atakayechukua nafasi ya uenyekiti , aweze kuvaa viatu vyangu vizuri kwani mzigo sio mdogo ni mzito huu,” amesema.

Akizungumzia uchaguzi mdogo wa KOHANI, Zanzibar ametoa wito kwa Tume Huru ya Uchaguzi kusimamia vizuri na kutenda haki na akasema kama wanaona inafaa ni vema mchakato huo ukasimama ili kupata idadi kamili ya wapiga kura ndipo uendelee.

“Niwaombe Tume ya Uchaguzi, sheria juzi imebadilishwa inaitwa Tume Huru ya Uchaguzi, maneno ni tofauti na vitendo tunataka tuone kweli wanafanya kazi kama tume huru, hivi sasa kuna watu Zanzibar wanapewa vitambulisho vipya vya kupiga kura.

“Tunawaambia tume kwani nini wasisimamishe mchakato huo katika Jimbo la KOHANI, ili tukapate idadi kamili ya wapiga kura ili tujue hawa ndio wapiga kura katika uchaguzi huu wa marudio na likimalizika hilo, mchakato huo uendelee ila wakifanya tofauti tutapata mashaka sana kama kweli tume itafanya kazi kwa uhuru.

“ Naiomba tume izingatie hili, ifuate sheria, taratibu pia wawe wawazi ili tuhakikishe uchaguzi huu unakuwa huru na haki ili watu wapate matumaini kwamba kweli tunayo tume huru ya uchaguzi vinginevyo tutakuwa na wasiwasi ule ule tuliokuwa nao siku zote,” amesema.

No comments:

Post a Comment