ASKOFU NGONYANI AZINDUA KITABU KIPYA KINACHOITWA KURUDI KWA YESU - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, August 21, 2024

ASKOFU NGONYANI AZINDUA KITABU KIPYA KINACHOITWA KURUDI KWA YESU


NA MAGENDELA HAMISI

MCHUNGAJI wa Kanisa la The Truth Ministry, Askofu Aurelian Ngonyani, amezindua kitabu chake kipya   kinachoitwa Kurudi Kwa Yesu chenye kurasa 225 ambacho tayari kimeanza kuuzwa kwa watu mbalimbali ndani na nje ya nchi.


Akizindua kitabu hicho, leo Agosti 21, 2024 jijini Dar es Salaam, Askofu Ngonyani amesema kuwa kitabu hicho kitauzwa kwa njia tatu tofauti ikiwemo ya sauti, nakala Tete (PDF) na Kitabu na tayari vimechakatwa na kuwekwa kwenye mifumo hiyo.


"Kitabu hiki chenye kurasa 225, nimekichakata na kukiweka katika mfumo wa sauti na PDF lengo ni kufanya hata wenye uono hafifu waweze kupata ujumbe.


Pia kila muhitaji atakuwa na uwezo wa kupata Kitabu kupitia kiganjani mwake kwa simu ya mkononi ya (smart phone), kwa mfumo mpya wa mtandao ambao nauzindua leo ambao utamuongoza kununua kitabu hicho," amesema.


Amesema sababu ya kuweka  kitabu hicho kwa njia tofauti ikiwemo ya sauti ni kutokana kubaini kupitia tafiti ndogo kuhusu usomaji wa vitabu na amebaini kuwa wasomaji WA vitabu NI wachache na wengine kutokuwa na miundombinu rahisi inayomwezesha kila mtu kuwa msomaji wa vitabu na kujiongezea maarifa.


Kulingana na hali hiyo, amefanikiwa kuunda rahisi wa uuzaji wa vitabu unaotumia msaada wa akili mnemba ambapo mtumiaji wa simu janja atapaswa kutuma neno' Hi' kwenda namba 0766111167.


Ameongeza kuwa baada ya hapo, mfumo umpeleka kwenye Duka la vitabu kidigitali 'Ngonyani Store' na kumuongoza kwa muongozo na kununua kitabu ambavyo vimechakatwa katika mifumo ya sauti na Nakala Tete (PDF).


Ameongeza kuwa maudhui ya kitabu hicho, ni muhimu mtu kuyapata kwa kuwa yanafunua misingi kuhusu maisha ya sasa na kinajibu maswali yanayoumiza vichwa vya watu wengi kama vile Kurudi kwa Yesu, kipindi cha Mpinga Kristo pamoja na kuweka wazi Matukio makuu ya taifa la Israel.


Alifafanua kuwa hadi kufanikiwa kuandika kitabu hicho, amefanya tafiti kwa kipindi cha miaka 20, pamoja na kufundisha katika chuo vya Theolojia ndani na nje ya nchi.


Pia amepata mafanikio makubwa kuandika kitabu hicho kutokana na kuongozi safari za mafunzo na tafiti katika nchi ambazo matukio yaliyoandikwa katika Biblia yaliyotokea.


Askofu Ngonyani amesema baadhi ya nchi hizo ni Misri, Jordan, Uturuki, Israel,Ugiriki, Ufaransa, Ureno na Italia kupitia kampuni yake ya AUMARK na tayari hadi sasa ameshaandika vitabu 10 vyenye mlengo tofauti na vipo madukani.




No comments:

Post a Comment