NA MWANDISHI WETU
UONGOZI wa Chama Cha ACT Wazalendo umesema kwamba wakati Taifa likielekea kuhitimisha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, 2024 umedai kubaini kasoro ambazo zinahitajika kufanyiwa kazi ikiwemo baadhi ya wagombea wao kutishiwa maisha.
Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Tanzania Bara, Isihaka Mchinjita ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam baada ya kufanya ziara ya kikazi katika maeneo mbalimbali nchini wakati huu taifa likiwa katika hatua za mwisho kwa ajili ya kuhitimisha uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
“Dosari hizi tulianza kuziona mapema kabisa na tukaziomba mamlaka husika kuzifanyia kazi na hadi sasa bado hakuna hatua ambazo zimachukulia na wakati tukielekea kujkamiliksha uchaguzi tumebainusha nyingine ikiwemo wagombea wetu kutishiwa maisha na kusababisha kushindwa kuchukua fomu,” amesema.
Ameongeza kuwa baadhi ya dosari nyingine ni baadhi ya wagombea wao kunyimwa fomu au kupewa fomu moja na nyingine mbili atanatikiwa kwenda kutoa copy jambo ambalo ni kinyume na utaratibu na wengine wakiladhimishwa kujitoa katika kinyang’anyilo cha uchaguzi.
Amedai changamotoa ya wagombea wao kutishiwa maisha imejitokeza katika baadhi ya majimbo ya mkoa wa Lindi na kusababiusha wagombea wao kushindwa kuendelea na mchakato kutokana na kuhofia maisha yao.
Pia baadhi ya wagombea wamekuwa wakitakiwa kuwa na kitambulisho cha Taifa kwa lengo la kuthibitisha uraia wao na kufafanua kuwa tofauti na hilo amedai kwamba katika Jimbo la Tunduma, Msimamizi wa Msaidizi alitoa fomu kwa mgombea wa ACT hasiyetambulika.
Amesema baada ya uongozi wa ACT, kulalamika kwamba mgombea wao, Emmanuel Mwawalo hajachukua fomu jambo hilo likapingwa vikali na msimamizi wa Mtaa wa Chapwa A katika Jimbo la Tunduma.
Mwandishi wa Magendela Blog, alimtafuta kwa njia ya simu Msimamizi Msaidizi hiyo ili kuthibitisha , simu haikupokelewa hivyo jitihada zinaendelea za kumtafuta ili athibitishe.
Aidha amedai katika Jimbo la Nyamagama jijini Mwanza,Kata ya Mabatini, katika Jimbo la Tandaimba wagombea wao walishindwa kuchukua fomu baada ya ofisi husika kufungwa, fomu zitolewa bila masharti na zirejeshwe.
Kutokana na kasoro hizo wametoa wito kwa Mamlaka husika iondoe wasimamizi ambao maeneo yao wamelalamikiwa, pia katika maeneo ambayo wasimamizi hawatoa fomu au kuwa na mgombea mmoja kwa sababu ya wengine kuzuiwa,uchaguzi usifanyike.
No comments:
Post a Comment