KAPINGA AENDELEZA MCHAKAMCHAKA KUHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, November 23, 2024

KAPINGA AENDELEZA MCHAKAMCHAKA KUHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA


NA MWANDISHI WETU, RUVUMA

MBUNGE wa Vijana Mkoa wa Ruvuma (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga anaendelea na kazi ya kuhamasisha wananchi katika maeneo mbalimbali ya mkoani humo ili waweze kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu.


Baada ya ziara ya mafanikio aliyoifanya wilayani Namtumbo, Kapinga amefanya ziara pia  wilayani  Mbinga kwa kuanza na Vijiji vya Mkako na Kigonsera  ambapo amewaasa wananchi kuchagua viongozi bora watakaosimamia shughuli za maendeleo katika Mitaa, Vijiji na Vitongoji hapa nchini.


"Wananchi mliopo katika Kata ya Kigonsera, Mkako na maeneo yote ya Mbinga ifikapo Novemba 27, 2024 jitokezeni kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa ili mchague viongozi makini kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM)." Amesisitiza Kapinga


Amesema lazima umakini uwepo katika uchaguzi wa Viongozi kwani ndio watakuwa wasimamizi wakuu wa miradi ya maendeleo kwenye maeneo ya Wananchi hivyo waangaliwe watu watakaoweza kuongoza wananchi kwa ufanisi pamoja na miradi ya maendeleo.


Pamoja na kuhamasisha Wananchi kushiriki katikaU chaguzi wa Serikali za Mitaa, Kapinga ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa maendeleo ngazi ya Taifa hadi Kitongoji kushirikiana na Serikali katika kuwafikishia  wananchi maendeleo na huduma bora  ikiwemo afya, elimu.




No comments:

Post a Comment