WAJAWAZITO 12,000 KUNUFAIKA NA MRADI WA LISHE WA MIL. 200/- ZANZIBAR NA BARA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Monday, December 22, 2025

WAJAWAZITO 12,000 KUNUFAIKA NA MRADI WA LISHE WA MIL. 200/- ZANZIBAR NA BARA


NA MWANDISHI WETU 

CHUO Cha Islamic Vocational Training Centre cha Unguja Darajani, Zanzibar kinatarajia kuwapa elimu ya lishe wanawake wajazito zaidi ya 12,000 kwa  lengo la kusaidia watoto wakazaliwa kuwa  na njema na kinga imara.
 
Mkuu wa Chuo hicho, DKT David Msuya  ametanabaish hayo leo, Disemba 22, jijini Dar es Salaam na kufafanua kwamba wataanza kutoa semina hiyo kisiwani Pemba Februari 10, 2026 na watakuwa na mikutano mitatu.

"Baada ya hapo tutakwenda kutoa semina hiyo kwa wakazi wa kisiwa cha Unguja na tutafanya hivyo Kwa kushirikiana na wataalam wa afya," amasema.

"Kwa sasa tuko tayari kwaajili ya kuanza mchakato huo tunachosubiri ni maelekezo kutoka Wizara ya Afya Zanzibar, ambayo itatoa wataalam tutakaombana nao na ndio hasa watakuwa mstari wa mbele kutoa elimu hiyo hiyo.

Pia amesema baada ya mafunzo hayo kukamilika visiwani Zanzibar wataendelea kutoa elimu hiyo Tanzania Bara katika Halmashauri ya mikoa Pwani, Bagamoyo, Iringa na Morogoro.

Dkt Msuya, amesema kwamba mradi unagharimu milioni 200 na utelezaji wake utashirikisha viongozi wa Serikali za Mitaa kwa Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar watshirikishwa Masheha ili kuhakikisha idadi ya kutosha inapatikana
 
Ameongeza kuwa wanaamini elimu wanayotarajia kuitoa Kwa wakazi hao itasaidia kuwaongezea maarifa wajazito namna ya kuwa na lishe bora wakati WA ujauzito ili watoto wataozaliwa wawe na afya njema.

Kwa mujibu wa Dkt.  Msuya wakati wa elimu pia itaenda sanjari na elimu ya magonjwa wa Kichocho na Utapiamlo ambayo yamekuwa yakiwakumba watoto wengi


No comments:

Post a Comment