NA MWANDISHI WETU
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Pwani, kwa kipindi cha Julai hadi Septemba, 2024
imefanikisha ukusanyaji wa shilingi bil 1.5 kati ya bil. 7.5 ya michango ya wafanyakazi kutoka kwa waajiri
waliokuwa hawaipeleki kwenye mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Imeelezwa kwamba kiasi hicho cha
fedha ni sawa na asilimia 103 ya makusanyo ambayo yamepatikana baada ya
TAKUKURU Mkoa wa Pwani kuingilia kati mfumo wa ukusanyaji michango ya watumishi
kwenda mifuko ya Hifadhi ya Jamii baada ya kubaini uwapo waajiri ambao walikuwa
hawapeleki michango kwa nia hovu au kwakutojua sheria.
Akizungumza leo Novemba 13, 2024 na
Waandishi wa Habari mkoani Pwani, Naibu Mkuu TAKUKURU wa mkoani humo, Alli Sadiki
, amefafanua kwamba sababu ya kuingialia mfumo huo ni baada ya kubaini uwepo wa
waajiri 77 kwa makusudi au kwa kutofahamu sheria walishindwa kupeleka michango
ya watumishi wao katika mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF.
Amesema jambo hilo limewanufaisha
waajiri hao na ingesababisha watumishi kushindwa kupata mafao stahiki kitu
ambacho si sawa na kusababisha TAKUKURU kulifanyia kazi na wadaiwa kukubali
kulipa deni la sh. 7, 505,723,317.10 kwa 20% ifikapo Julai, 2024.
Naibu Mkuu huyo wa Takukuru
mkoani Pwani, amesema kwamba baada ya kufutilia na kusimamia sheria za mifuko
ya Hifadhi pamoja na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11/2007 , Julai
17, mwaka huu walifanikiwa kufanikisha makusanyo yaliyofikia Sh. 1,
543,125,427,00 yakiwa ni sawa na 103% kwenda NSSF.
Ameongeza kuwa kutokana na
mchakato huo kufanyika waajiri hao 77, wamesema kwamba wapo tayari kushirikiana
na TAKUKURU kuendeleza mapambano dhidi ya rushwa na awali changamoto hiyo
ilijitokeza kwa kuwa hawakuwa na elimu ya makosa ya rushwa kwa mujibu wa Sheria
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini na Makosa ya Mifuko ya Hifadhi ya
Jamii.
Ameibainisha kwama baadhi ya
waajiri hao hawakuwa wanajua kuwa kutokupeleka michango kwa wakati NSSF ni kosa
kisheria, Pia baadhi ya waajiri walikuwa hawapeleki michango kwa makusudi na
kusababisha kuvunja Sheria na baada ya kupewa maelekezo walichanga bila shida.
“Nia ovu ya baadhi ya waajiri ilisababisha
kupoteza fedha za za watumishi wao na kujinufaisha kwa kutowalipa michango NSSF
na baadae ingesababisha wahusika kutopata mafao kama stahili, amesema.
Ameongeza kuwa katika kipindi
hicho, pia wamefanya semina 53, mikutano ya hadhara 39, vipindi vya Redio 3,
Kuimarisha Klabu za Wapinga Rushwa 53, Uandishi wa Makala 8 na TAKUKURU Rafiki
3.
Aidha amefafanua kuwa katika
kipindi tajwa,wameendelea na utekelezaji wa Programu ya TAKUKURU Rafiki na
kuzifikia jumla ya Kata Sita na kero mbalimbali zilizoibuliwa na kupatiwa
ufumbuzi zikiwemo kutoka Idara ya Ruwasa, Halmashauri, Afya, TFS, Elimu na
TANROADS.





No comments:
Post a Comment