ZITTO KABWE ATOA MIFUKO 300 YA CEMENT LUDEWA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, November 13, 2024

ZITTO KABWE ATOA MIFUKO 300 YA CEMENT LUDEWA


NA MWANDISHI WETU

KIONGOZI Mstaafu wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe, ametekeleza ahadi ya kutoa msaada wa Cement mifuko 300 kwa Kata ya Ruhuhu, Kijiji Cha Ngerenge Mkoani Njombe kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari katika Kata hiyo.


Mifuko hiyo yenye thamani ya shillingi milioni 6.6 imekabidhiwa kwa niaba ya Zitto kijijini hapo na Katibu wa Idara ya Haki za Binaadamu na Vyombo vya Uwakilishi wa Wananchi Taifa ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria wa ACT Wazalendo mbele ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndg. Sunday Deogratus, Diwani wa Kata hiyo inayoongwa na ACT Wazalendo, Atanas Titus Haule Sanga (Magamba) na viongozi wa Chama Mkoa, Jimbo na Wananchi. 


Ahadi hiyo ya KCM ilitolewa katika Ziara ya Chama iliyofanyika August mwaka huu kwa ajili ya kutatua changamoto ya ukosefu wa Shule ya Sekondari katika Kata hiyo. Tayari ujenzi wa Shule hiyo umeanza kwa nguvu ya Wananchi, Halmashauri na Wadau mbalimbali. 


Mkurugenzi wa Halmashauri na Diwani Sanga kwa nyakati tofauti wametoa shukrani zao kwa KCM na kutoa wito kwa Wadau mbalimbali Nchini kuchangia juhudi hizo.

Kata ya Ruhuhu ipo pembeni ya Ziwa Nyasa mpakani mwa Tanzania na Malawi.




No comments:

Post a Comment