MAMA ONGEA NA MWANAO YATOA VIFAA KWA WAHITAJI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, December 31, 2024

MAMA ONGEA NA MWANAO YATOA VIFAA KWA WAHITAJI


MWANDISHI WETU

TAASISI ya Mama Ongea na Mwanao, imeshiriki katika kongamano kwa kutoa huduma tiba kwa  makundi mbalimbali ya watu wenye mahitaji maalumu pamoja na wakazi wa Dar es Salaam.


Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Desemba 31, 2024 katika kongamano maalumu katika Ukumbi wa Karimjee ambapo mgeni rasmi ambaye ni Meya wa Jiji hilo, Omari Kumbilamoto amesema tuuige mfano huu kutoka kwa steve Nyerere.


"Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao ambapo Steve Mangele ambaye ni Mwenyekiti, inafaa kuiga hayo anayoyafanya kwa kuwasapoti watu wenye ulemavu kwa kutoa zawadi mbalimbali," amesema. 


Aidha Kumbi la moto amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania imejipambanua kuhakikisha inatoa kiasi cha shilingi billion 5 kwa kundi la wenye ulemavu.


Nae Mwenyekiti wa hiyo, Steven Mengele 'Steve Nyerere', amesema kundi hilo ni muhimu sana na mwaka huu ni mwaka wa tatu toka kuazishwa kwake limeonekana kufanya vizuri sana na wametoa,.where chair 25,jezi na mipira


"Rais wetu Mama Dkt.Samia ameamua kulishika mkono ambapo litatembea maeneo mbalimbali ya Tanzania kwa kila mkoa kuhakikisha wanakutana na watu wenye uhitaji kwa kuwapa Zawadi mbalimbali ikiwemo viti  mwendo 50, pamoja na kukarabati madarasa yao," amesema.


Pia ameliangalia kwa macho mawili kundi hili kuhakikisha wahitaji hawa wananufaika na mambo kemkem hivyo aliona ni nyema kushea nao kula nao pamoja kucheza nao.


"Nawashukuru wote mlioalikwa siku ya Leo taasisi ya mama ongea na mwanao kupitia kwa Rais wetu itahakikisha inashiriki na waendesha vikoba kwa kuwapatia kiasi cha shilingi milioni tano kwa kila kikundi cha wahitaji hawa," amesema.



No comments:

Post a Comment