MTOTO WA 'SNAKE MAN' KUZICHAPA NA MNAMIBIA FEB 28 MWAKA HUU - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, February 25, 2025

MTOTO WA 'SNAKE MAN' KUZICHAPA NA MNAMIBIA FEB 28 MWAKA HUU


NA MWANDISHI WETU


BONDIA Amiri Matumla, February 28 mwaka atapanda ulingoni katika Ukumbi wa Magomeni Sokoni dhidi ya mpinzani wake kutoka Namibia, Paul Amavila.


Hayo yamebainishwa leo, Feb 25, 2025 na Mkurugenzi wa Mafia Boxing Promotion, 'Knock Out ya Mama' Ally Zayumba na kufafanua kwamba bondia huyo katika pambano hilo atazichapa  na mpinzani wake kwa mizunguko nane.


'Hili ni pambano lake la kwanza tangu ajiunge kwenye mapambano ya ngumi za kulipwa na ameahidi kufanya vizuri kwa lengo la kuanza kutenge rekodi nzuri katika karia yake kupitia masumbwi, amesema.


Zayumba ameongeza kwamba siku hiyo pambano hilo kutakuwa na mapambano mengine 11 ya utangulizi yakiongozwa na mkongwe Dullah Mbabe.


Pia amesema kuwa huu ni msimu  tatu Kwa mapambano ya aina hiyo kufanyika chini ya Mafia Boxing Promotion yakiwa na lengo la kunadi miradi iliyotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.


Amefafanua kwamba Michezo wa ngumi katika kipindi hiki cha uongozi wa Rais Dkt Samia,  umekuwa na mafanikio makubwa hivyo ni vema watanzania wakaendelea kumuunga mkono.


Pia amesema viingilio vitakuwa ni shilingi, 50,000, sh. 20000 na 10,000 na mabondia wote watapima uzito katika Ukumbi huo Feb 27, mwaka huu.


Zayumba ametaja mabondia wengine watakaopanda ulingoni katika mapambano ya utangulizi ni Oscar Richard atakayezipiga na bondia kutoka Malawi.


Rashid Mtange kutoka Nacoz Camp chini ya kocha Ramadhani Uhadi 'Rama Jah' atazichapa na bondia kutoka India na  wengineo.


 Naye Bondia Matumla, ambaye ni mtoto wa Rashid Matumla' Snake Man' amejinasibu kufanya vizuri pambano hilo kutokana na kupata maandalizi ya kutosha.


'Naomba watanzania wajitokeze kwa wingi kuja kushuhudia pambano hilo ambalo litakuwa na burudani ya aina yake, amesema.

No comments:

Post a Comment