VETA YAENDELEA KUCHANGIA UBUNIFU NA MAENDELEO YA UFUNDI STADI NCHINI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, March 20, 2025

VETA YAENDELEA KUCHANGIA UBUNIFU NA MAENDELEO YA UFUNDI STADI NCHINI

 


NA MWANDISHI WETU

WAZIRI Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, amesisitiza kuwa VETA imechangia pakubwa katika kukuza ubunifu nchini, ambapo awali ubunifu wa hali ya juu ulionekana tu kwa mataifa yaliyoendelea.

Akizungumza Machi 20, 2025, katika mjadala wa wadau wa VETA uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam, Pinda amesema mchango wa Mamlaka hiyo haupaswi kubezwa, bali unahitaji kuimarishwa zaidi.

Pinda ameeleza kuwa VETA imekuwa chachu ya kuzalisha wahitimu bora ambao wanakubalika katika soko la ajira, ndani na nje ya nchi. Alisema, “Ni ukweli usiopingika kwamba VETA imetoa mchango mkubwa sana katika Taifa hili, na hakuna namna unaweza kuepuka ufundi stadi katika maisha yako kama binadamu.”

Aidha, Waziri Mkuu Mstaafu ametembelea mabanda mbalimbali ya VETA na kujionea kazi za ubunifu zinazofanywa na vijana waliopitia mafunzo ya ufundi stadi, ambapo aliipongeza VETA kwa juhudi zake katika kuleta maendeleo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore, amesema mafanikio yanayoonekana leo ni matokeo ya juhudi zilizowekwa wakati wa uongozi wa Pinda.

Maadhimisho ya miaka 30 ya VETA yatafikia kilele kesho, Machi 21, 2025, ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, atahitimisha rasmi sherehe hizo.

No comments:

Post a Comment