WANYAMAPORI WAPAMBA SIKU YA MISITU DUNIANI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, March 20, 2025

WANYAMAPORI WAPAMBA SIKU YA MISITU DUNIANI

NA JOHN MAPEPELE

KWA mara ya kwanza  katika historia ya maadhimisho ya Siku ya Misitu Duniani ya mwaka huu  hapa nchini yanayofanyika katika viwanja vya Saba Saba Mjini Njombe  Wizara ya Maliasili na Utalii imeandaa maonesho maalum ya mnyororo wa thamani wa sekta ya misitu pamoja na Wanyamapori.


Kwa vipindi tofauti wakikagua maandalizi ya siku ya Misitu Duniani kwenye maonesho Waziri wa Maliasili na Utalii, Pindi chana na Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbasi wamefafanua kuwa Serikali imeamua kuwaleta Wanyamapori katika maonesho hayo ili kutoa hamasa kwa wananchi kupenda utalii wa ndani.


" Tanzania imebarikiwa kuwa na eneo kubwa la misitu takribani asilimia 50 ambalo ni makazi ya Wanyamapori, hivyo tumeamua kuwaleta wanyama  wananchi waweze kupenda kutembelea hivyo kuliingizia taifa letu fedha." Amepongeza  waziri 


Naye Dkt. Abbasi amewaarika    wananchi  kutembelea maonesho ya Wanyamapori  hao na kwamba  Serikali imetoa fursa ya wanyama hao kuendelea kuwepo katika viwanja hivyo katika siku za mwisho wa juma hata baada ya kilele hapo kesho ili wananchi wengi wapate fursa ya kuwaona.


Mgeni rasmi hapo kesho ni Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Kauli mbiu ya kitaifa ya mwaka huu ni ongeza thamani ya mazao ya misitu kwa uendelevu wa raslimali kwa kizazi hiki na kijacho.






No comments:

Post a Comment