MSHINDI TUZO YA TAIFA MWALIMU NYERERE UANDISHI BUNIFU 2025 KUZOA MIL 10 - MAGENDELA BLOG

Recent-Post

ads header

Monday, April 7, 2025

MSHINDI TUZO YA TAIFA MWALIMU NYERERE UANDISHI BUNIFU 2025 KUZOA MIL 10


Prof. Adolf Mkenda (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu zitakofanyikaAprili 13, 2025 ikiwa ni kumbukizi ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

 NA MWANDISHI WETU


MSHINDI wa Tuzo za Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu, 2025 ataondoka na kitita cha Shilingi milioni 10, taslimu pamoja na cheti.


Wakati mshindi wa pili atajinyakulia kitita cha sh. mil 7, watatu ataondoka na sh. mil 5 na washindi wanne hadi wa 10 watapata cheti.


Pia imeelezwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya tuzo hiyo inayofanyika jijini Dar es Salaam kwa mara ya nne tangu kuanzishwa kwake , atakuwa Makamu Rais wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango.


Hayo yamebainishwa leo, Aprili 7, 2025  jijini Dar es Salaam na Waziri wa Elimu na Sayansi na Teknolojia Prof.  Adolf Mkenda na ametanabaisha kwamba maandalizi yote yamekamilika kwa asilimia kubwa na kinachosubiriwa na siku hiyo ya tukio kubwa kufika.


Aprili 13 kila mwaka ndio siku ya kumbukizi ya kuzaliwa, Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere na ndio imepangwa kufanyika kwa tuzo hiyo na huu ni msimu wa nne.


 

"Mgeni rasmi kuwa ni makamu wa Rais inadhihirisha namna Serikali inavyotambua na kuweka uzito katika tuzo hiyo ya Uandishi Bunifu ambayo kwa njia moja ama nyingine inasaidia kukuza lugha ya Kiswahili kutokana na Waandishi shindani kutumia lugha hiyo katika kazi zao" amesema.


Profesa Mkenda amesema kuwa Tuzo ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu ni miongoni mwa njia bora za kuenzi fikra, falsafa na maono ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ambaye aliweka msingi wa matumizi na ukuzaji wa lugha ya Kiswahili kama nyenzo ya elimu, umoja na maendeleo ya jamii ya Watanzania.


“Tuzo hii ni heshima kwa Mwalimu Nyerere lakini pia ni jukwaa mahsusi kwa waandishi chipukizi na wakongwe kuonesha umahiri wao katika nyanja mbalimbali za uandishi kama vile riwaya, ushairi, hadithi za watoto na tamthiliya,” alisema.

Pia amesema mshindi wa kwanza licha ya kushinda mil 10, kazi yake itachapishwa  na kutumika katika shule na maktaba nchini kwa ushirikiano na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET).


Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo, Profesa Penina Mlama ametanabausha kwamba majaji wamekamilisha kazi ya kusoma miswada iliyowasilishwa na tayari orodha teule ya waandishi waliopendekezwa imechapishwa. 


Ameongeza kuwa hadi sasa tayari zimechapishwa kazi mbili za washindi na kazi ya tatu ipo katika hatua za mwisho kukamilika.

 

No comments:

Post a Comment