TUMIENI MITANDAO YA KIJAMII KUTAFUTA FURSA ZA AJIRA - MBWAMBO - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, April 5, 2025

TUMIENI MITANDAO YA KIJAMII KUTAFUTA FURSA ZA AJIRA - MBWAMBO

 


NA MWANDISHI WETU


WAHITIMU  104 wa Chuo Cha Ufundi Veta -  Furahika wameaswa kutumia mitandao ya kijamii kwaajili ya kutengeneza mtandao ajira na si vinginevyo.


Wito huo umetolewa leo, Aprili 4, 2025 jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoani humo, Mwajabu Mbwambo, wakati wa mahafali ya 19 ya chuo hicho.


"Wapo baadhi ya wahitimu wanaweza kutumia mitandao kuposti matukio yao ya starehe jambo ambalo haliwasaidii, hivyo ni vizuri mkaitumia kwaajili ya kutafuta 'connection' ya ajira kupitia makundi ya Whatsaap," amesema.


Pia amewasisitiza wahitimu hao kuwa na hofu ya Mungu jambo litakalowasaidia kuepuka kujiingiza katika vitendo viovu.


Tofauti na hayo, pia Mbwambo aliwataka wahitimu hao kuwa mabalozi wazuri wa chuo kwa kuwa wavulivu na waadilifu  katika maeneo yao ya kazi jambo litakalosaidia chuo kuendelea kuaminika kwa wadau mbalimbali wa maendeleo.


Mbwambo pia, hakusita kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuwezesha mpango wa Elimu Bure kwa kundi hilo la vijana ambao walishindwa kuendelea na masomo kutokana na changamoto mbalimbali.


Chuo hicho kinatoa elimu bure chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, ikiwa ni juhudi ya Serikali ya Awamu ya Sita kutoa kozi za muda wa miezi mitatu hadi mwaka mmoja.


Kozi ambazo chuo hicho kinatoa ni udereva, utalii, ususi, urembo, ukondakta wa mabasi, umeme n.k.


Naye Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Dkt David Msuya, amewataka wahitimu hao kuacha uvivu katika majukumu yao ya masomo kwa vitendo ili iwe sehemu ya kujiweka karibu na kupata ajira.

 

Pia amewaasa kuwa na nidhamu katika kazi na kuachana na tabia za kihuni zitakazowaweka kwenye dosari katika utafutaji ajira.


"Wapo baadhi ya wahitimu, walipata eneo la kufanyia masomo kwa vitendo cha kushangaza walipigania mwanaume wakiwa kazini jambo lililofanya kutia doa chuo chetu, sasa nyinyi msiwe wa aina hiyo, mkawe wema na mabalozi wazuri," amesema.


Naye mhitimu wa chuo hicho, Winfrida Salum, amesema ataitumia vizuri elimu aliyoipata kwaajili ya kutafuta mafanikio.


Pia Biko Benjamin muhitimu wa kozi ya hoteli, amesema kutokana na elimu aliyoipata ataitumia vizuri katika soko la ajira nchini Kwa kuajiriwa au kujiajjri




No comments:

Post a Comment