MATAIFA 15 YAKUTANA JIJINI DAR KUJADILI MABORESHO MKATABA VYANZO VYA NYUKLIA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Monday, June 23, 2025

MATAIFA 15 YAKUTANA JIJINI DAR KUJADILI MABORESHO MKATABA VYANZO VYA NYUKLIA


NA MWANDISHI WETU

MATAIFA 15 ya Ukanda wa Afrika yamekutana jijini Dar es Salaam kujadili mkataba wa kulinda matumizi ya vyanzo vya nyuklia ambavyo vikitumika vizuri vitakuwa na faida kwa nchi husika



Majadiliano hayo yamefanyika leo Juni 23, 2025 ambapo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Sayansi na Teknolojia, Daniel Mushi amesema wamekutana kujadili mkataba huo ambao ni muhimu kwa sababu nyuklia ikitumika vizuri ina faida lukuki.



Pia amefafanua kwamba wamekutana kujadili maboresho ya mkataba ili kila nchi iweze kutekeleza na kuongeza uelewa kwa nchi wanachama.


Ameongeza kuwa mkutano huo umeandaliwa na Wakala wa Nguvu za Nyuklia na Atomu na kushirikisha wageni kutoka nchi mbalimbali duniani na hiyo ni hatua moja muhimu ya kulinda vyanzo vya nyuklia ili visiwe na madhara kwa binadamu bali nchi yetu ifaidike.



"Serikali imeshaweka nia ya kutengeneza umeme wa nyuklia ili nchi yetu isitegemee umeme wa maji,mikakati yake Iko tayari kwa ajili ya mpango huo na wataalam wanasomeshwa kwa ajili ya mpango huo  wamaendelea Ili watanzania waweze  kunufaika.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Nguvu za Atomu Tanzania,Najat Nasibu Mohamed ameeleza kuwa kuna hatua mbalimbali zimeandaliwa na Wakala wa nguvu za atomu Duniani ambapo inaweza  kwa vyanzo vikubwa vinaweza kuchukua miaka kumi na vyanzo vidogo miaka Saba ama mitano



Pia ameeleza kwamba  Kuna vyanzo mbalimbali  na teknolojia inabadilika kwa Kasi Kwa Sasa Kuna vyanzo vidogo vidogo ambavyo happo nyuma havikuwepo Kwa Sasa tunaweza kuchukua muda mfupi na nchi yetu inakua kiuchumi na ongezeko la watu.


Aliendelea kwamba mkutano huu ni fursa ya kupeana  uzoefu, mikakati na kuhamasisha Tanzania na nchi  15 za Afrika waweze kusaini mkataba huo na kuona umuhimu.


Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Atomu Jiohn Sambichaka amesema kwamba wanashirikiana na Wakala wa Tume za Atomu Duniani.


Ameongeza kuwa lengo la mkutano huo kupeana uzoefu jinsi yakufahamu taratibu za usafirishaji madini ya nguvu za Atomu ambazo yake yanatumika sehemu mbalimbali katika matumizi.


No comments:

Post a Comment