WATANZANIA WAHAMASISHWA KUSOMA MASOMO YA UBAHARIA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, July 8, 2025

WATANZANIA WAHAMASISHWA KUSOMA MASOMO YA UBAHARIA


 NA MAGENDELA HAMISI

KUTOKANA  na kuwepo uhaba wa Wataalamu katika sekta ya Bahari hapa duniani kote, watanzania wamehamasishwa kusoma masomo hayo ili kupata watanzania wengi wenye fani ya ubaharia ambao wataweza kusambaa katika mataifa mbalimbali na kupata ajira


Mohamed Salum ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa  Shirika Wakala wa  Meli Tanzania (TASAC ), amebainisha hayo leo Julai 7, 2025 jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) ambapo Tasac wakiwa miongonj mwa washiriki.


Mkurugenzi Mkuu huyo amesisitiza kwamba kwa sasa duniani kwa  ujumla bado kuna upungufu wa mabaharia hivyo ni wakati sahihi kwa watanzania kutumia fursa hiyo kusoma masomo ya fani hiyo.



" Ni vizuri sasa watanzania wakatumia fursa hiyo, kusoma masomo yanayohusu sekta ya bahari jambo litakalosaidia kupata mafunzo ya kitaalamu kuhusu ubahari kwani soko bado linahitaji Wataalamu hao" amesema.



Akifafanua kuhusu ushiriki wa TASAC katika maonesho hayo, wapo hapo kwa ajili ya kuhamasisha na kutoa elimu kuhusu fursa zilizo katika sekta hiyo na umuhimu wake.



Pia akiweka wazi majukumu ya TASAC amefunguka kwamba miongoni mwa majukumu yao ni  kusimamia mambo yanayohusu usalama wa bahari,  meli,  maeneo ya bandari na utekelezaji  wa Mkataba wa Usalama wa Meli na maeneo ya bandari(ISPS Code).


"Kazi ya TASAC  ni pamoja na kukagua  vyombo vya usafiri  majini, masuala ya kiusalama bandarini na  kudhibiti uchafuzi wa mazingira majini  unaosababishwa na vyombo vya usafiri majini,"amesema.


Aidha ameweka wazi kuwa majukumu yao mengine ni kusimamia shughuli za bandari kutoa  vibali  eneo linalofaa  na lisilofaa kwaajili ya Ujenzi wa bandari.


No comments:

Post a Comment