WAZIRI MKUU AKABIDHI TUZO YA UMAHIRI KWA MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO WIZARA YA NISHATI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Monday, July 14, 2025

WAZIRI MKUU AKABIDHI TUZO YA UMAHIRI KWA MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO WIZARA YA NISHATI


NA MWAMDISHI WETU 

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Jana  13 Julai, 2025 amemkabidhi Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Nishati, Neema Chalila Mbuja tuzo ya umahiri kufuatia mchango wake  alioutoa wakati wa Maonesho ya Dunia ya Biashara ya Osaka nchini Japan kwa upande wa Mawasiliano na kuitangaza nchi.


Majaliwa amempongeza  Mbuja wakati wa kilele cha  Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama Sabasaba 2025.


Sambamba na hilo.Majaliwa amempongeza Mbuja kwa kuwa muongozaji wa shughuli na kuwa mahiri wakati wa Kongamano la Kimataifa la Biashara, Uwekezaji na Utalii kwenye Maonesho ya Osaka Expo 2025.


Kwa upande wake Mbuja amemshukuru Majaliwa kwa kukabidhi tuzo hiyo iliyotolewa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara TANTRADE na kuahidi kuendelea kuitangaza Wizara ya Nishati Kimataifa.

                    



No comments:

Post a Comment