MGOMBEA URAIS KUPITIA NLD KUPOKEWA KWA KISHINDO AGOSTI 31,2025 JIJINI DAR - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, August 29, 2025

MGOMBEA URAIS KUPITIA NLD KUPOKEWA KWA KISHINDO AGOSTI 31,2025 JIJINI DAR


NA MWANDISHI WETU

BAADA  ya kuteuliwa rasmi na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, mgombea wetu wa urais kupitia chama cha National League for Democracy (NLD), Doyo Hassan Doyo, akiambatana na mgombea mwenza wake Bi. Chausiku Khatibu Mohamed, watawasili jijini Dar es Salaam Agosti 31, 2025.


Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano ya Umma, NLD,  Pogora Ibrahimna meaema mapokezi rasmi yatafanyika katika Makao Makuu ya Chama, Tandika, Dar es Salaam na yataudhuriwa na viongozi waandamizi wa chama, wanachama na wananchi mbalimbali.


"Tunawaalika.viongozi wa wilaya zote za NLD kutoka Mkoa wa Dar es Salaam, Wananchi kutoka mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.


"Waandishi wa habari na vyombo vyote vya habari, kuhudhuria kwa wingi katika mapokezi haya muhimu ya mgombea wetu na mgombea mwenza wake", imesema


No comments:

Post a Comment