![]() |
NA MWANDISHI WETU
KATIKA kipindi cha miaka minne ya SERIKALI ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, Bodi ya Michezo ya Lubahatisha inajivunia kukusanya Shilingi Bil. 260.21.
Akizungumza leo katika mkutano na Wahariri na Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari, Kaimu Mkurugenzi wa GBT, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa GBT, Olesumayan, amesema kabla ya hapo walikusanya sh. bil bilioni 131.99 na wanakadiria kipindi kichacho watafikia bilioni moja.
Katika mkutano huo ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa GBT, Olesumayan aliongeza kuwa katika makusanyo ya kodi ya zilikisanywa sh. bil 922.25 na ajira ambazo zimetolewa katika sekta hiyo ni zaidi ya 30,000.
Aidha amesema katika kipindi cha mwaka 2024/2025, GBT imetoa leseni ya Bahati Nasibu ya Taifa kwa kampuni ya Ithuba Tanzania Limited, inayomilikiwa na Watanzania kwa asilimia 40 na wawekezaji kutoka Afrika Kusini kwa asilimia 60.
Kampuni hiyo imewekeza zaidi ya USD milioni 20 (sawa na shilingi bilioni 50) na imeanza rasmi shughuli zake mwezi Aprili 2025.
Pia amebainisha kuwa michezo ya kubahatisha ni burudani, siyo ajira, hivyo washiriki wanapaswa kucheza kwa nidhamu bila kuhatarisha maisha yao kifedha.
Aliongeza kwamba asilimia tano ya mapato ya bodi hutumika kuendeleza michezo nchini. Hadi sasa, kati ya shilingi bilioni 44 hadi 53 zimetolewa kwa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya michezo.
GBT pia imesajili kampuni 62 zenye michezo ya kubahatisha 8549, lakini changamoto kubwa imebaki kwa waendeshaji wasio na leseni. Hatua zimechukuliwa kuhakikisha watoto hawashiriki kabisa katika michezo hiyo.
Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, kiasi cha shilingi bilioni 66.7 kimeingizwa nchini kutoka kwa wawekezaji wapya katika sekta hiyo.





No comments:
Post a Comment