NA MWANDISHI WETU, CHALINZE.
MKE wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mama Salma Kikwete amewaomba Watanzania kumpigia kura za kishindo mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk Samia Suluhu Hassan.
Aidha amemuombea kura Mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze Wilaya ya Bagamoyo kupitia CCM Ridhiwani Kikwete.
Mama Salma Kikwete ambaye alimwakilisha Rais Mstaafu Dk Jakaya Kikwete aliomba kura kwa wagombea hao wa CCM kwenye uwanja wa Mdaula wakati wa uzinduzi wa kampeni za Ubunge wa Jimbo la Chalinze.
Alisema kuwa Rais Mstaafu Dk Kikwete hakuweza kufika kutokana na majukumu mengine ya kitaifa lakini anaomba Watanzania wampigie kura kwa wingi mgombea Urais wa CCM ,Mbunge wa Chalinze, wabunge wote pamoja na Madiwani.
"Rais Mstaafu ameomba Oktoba 29 wote waliojiandikisha wakapige kura za kutosha kwa mgombea wetu wa Urais, Ridhiwani wabunge wengine na Madiwani wote 15 wa CCM wa Kata zote za Jimbo la Chalinze na nchi nzima,"alisema Mama Salma.
Alisema kuwa Rais aliyofanya kwenye Wilaya ya Bagamoyo ni makubwa sana na tusipompa kura asilimia 100 tutakuwa hatujamtendea haki kwani kafanya kazi kubwa sana na fursa zilizofunguka ni kielelezo cha utekelezaji wa ilani.
Alisema kuwa fedha nyingi zilizopatikana kupitia mapato ya ndani kumesaidia kuleta maendeleo kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Hospitali ya Wilaya ambapo Halmashauri ili kiasi cha shilingi bilioni 3 na serikali ikatoa kiasi cha shilingi bilioni 7 na baadhi ya majengo yamekamilika na mengine yanaendelea kujengwa.
Naye Mgombea huyo wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete alisema kuwa anachowaomba wananchi Oktoba 29 hakikisheni mnakipa imani chama kwa kumpigia Rais ambaye ni mgombea wa nafasi hiyo na anapata kura kwa asilimia 100 na mimi Mbunge na Madiwani nao wanashinda kwa kushindo.
"Moja ya changamoto ambazo nitazifanyia kazi endapo nitachaguliwa ni maji ili ifike asilimia 100 na maji kufika kwa wananchi majumbani badala ya kwenye vioski na kuzifikia kaya 300,000,"alisema Kikwete.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Pwani Zainabu Vullu alisema kuwa Rais Dk Samia Suluhu Hassan ni Mwanadiplomasia mahiri duniani na ameahidi akichaguliwa kupitia ilani ya 2025-2030 atahakikisha anaboresha huduma za afya, elimu, miundombinu
Vullu alisema kuwa Madiwani waliopita bila kupingwa tutoe elimu ya kupiga kura na kuchagua wanaccm msichague wasiotokana na ccm kwani wakiwapa wengine wasiotokana na CCM wataharibu.
Kwa upande wake Mratibu wa kampeni kanda ya Pwani Richard Kasesela alisema kuwa watu waliojiandikisha wahakikishe wanajitokeza kuwapigia kuwa wagombea wa CCM.
Kasesela alisema kuwa mwanaccm ahakikishe anaambatana na wenzake wawili kwenda kupiga kura kwa wagombea wa CCM na wasipopiga kura au kupigia wagombea wa vyama vingine ni kufanya usaliti.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bagamoyo Abubakar Mlawa alisema kuwa chama kimejipanga kuhakikisha Rais anapata kura za kishindo sambamba na Wabunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete na Bagamoyo Subira Mgalu na Madiwani wa Kata 15 za Chalinze.
Mlawa pia alitumia nafasi hiyo kuwakabidhi ilani Madiwani wa Kata 15 za Jimbo la Chalinze ili wakaitekeleze kwenye Kata zao ambapo Madiwani 12 wamepita bila ya kupingwa.





No comments:
Post a Comment