MGOMBEA UDIWANI PUGU STESHENI AZINDUA KAMPENI KWA KISHINDO ATOA AHADI LUKUKI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, September 16, 2025

MGOMBEA UDIWANI PUGU STESHENI AZINDUA KAMPENI KWA KISHINDO ATOA AHADI LUKUKI



NA HAMISI MRISHO 

MGOMBEA Udiwani Kata ya Pugu Stesheni, Salumu Shaibu  amezindua kampeni zake kwa kishindo akiahidi kusimamia vema Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuwaondolea kero wananchi wa Kata hiyo.

 Katika uzinduzi huo ambao umefanyika jana, Septemba 15, 2025 katika kata hiyo ya Pugu Stesheni amesema atasimamia vyema miradi ya maendeleo iliyopo kwa kufuata Ilani ya CCM.


Ameongeza kuwa miradi ambayo anakwenda kusimamia vema ni ujenzi wa kituo cha Afya itakayokuwa ya ghorofa mbili, miundombinu ya barabara na masoko.


Aidha ameahidi kusimamia miradi ya masoko moja litajengwa, Pugu Stesheni jambo litakalosaidia kupunguza kero kwa wakazi w eneo hilo kutembea umbali mrefu kwaajili ya kufuata mahitaji ya sokoni.


"Kwa upande wa miundombinu tutajenga barabara zetu kwa kiwango cha lami ikiwemo ya Pugu Mnadani kwenda Kifuru na nyinginezo Kwa changarawe na sehemu za vivuko zitajengwa vema ili zisiwe korofi hata kipindi cha mvua.

Barabara nyingine ambayo ameahidi kusimamia vema ili itengenezwe kwa kiwango cha lami ni kutoka Pugu Kajiungeni kwenda Pugu Mnadani na Mnadani kwenda Gongalamboto.

"Pia nitasimamia urasimishaji wa makazi yetu ili tuwe na uhakika na sehemu za kuishi pamoja na kutumia hati kwa ajili ya kuombea mikopo," amesema.

Aidha amesisitiza kwamba kipindi cha nyuma kulikuwepo na mchakato wa utoaji mikopo na kutokana na changamoto ya ulipaji ilisimamishwa, hivyo katika uongozi wake vikindi vyote vyenye sifa vitapewa mikopo bila ubaguzi hususan Kwa makundi maalumu.

Ameongeza kuwa anafahamu kwamba uongozi ambao umepita umefanya mengi ya kupongeza ikiwemo ujenzi wa Tanki la Maji Bangulo ambao umesaidia baadhi ya kata hiyo kupata maji safi na salama na changamoto ambazo zimesalia atahakikisha katika uongozi wake anazimaliza.

Kwa upande wake Mratibu wa kampeni za mgombea huyo,  Juma Mizungu ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa Vijana Wilaya ya Ilala amesema kuwa watu waliojiandikisha wahakikishe wanajitokeza kuwapigia kuwa wagombea wa CCM.


Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Ilala, Mwinyimkuu Singalaza amesema kuwa chama kimejipanga kuhakikisha Rais anapata kura za kishindo sambamba na Mbunge wa jimbo hilo na madiwani

"Tumejipanga vizuri kuhakikisha CCM inashinda na kutokana na idadi ya wanachama wetu waliopo katika kata hii kila mmoja anashawishi asiyemwanachama wetu watatu wakakipigie chama chetu hiyo itafanya tupate ushindi wa zaidi ya aslimia 80, amesema.

Amesema kuwa CCM ndio chama kinacholeta maendeleo na amani nchini kutokana na kuaminika kwake, hivyo wananchi wasipoteze muda wao kuchagua vyama vingine.

Naye diwani aliyemaliza muda wake, Shabanj Mussa, amesema kwamba hana kinyongo baada ya kushindwa kupenya kwenye kura za maoni na sasa yuko pamoja na mgombea kuhakikisha CCM inashinda Kwa kishindo katika Uchaguzi Mkuu ujao.

"Yapo maneno mengi yanasemwa kuwa nimejiweka pembeni baada ya kura zangu kutotosha, sasa niwaambie kwamba Mimi ni mwanachama niliyetokana na CCM, hivyo chaguzi za ndani zimekwisha kinachofanyika sasa ni kutafuta kura kwa ajili ya ushindi wa CCM ni si vingine.

Nitasimama mtaa kwa mtaa, nyumba Kwa nyumba, Mkutano hadi Mkutano kuhakikisha mgombea wetu wa udiwani, ubunge na urais wanapata kura za kutosha na ninawaomba wananchi kujitokeza Kwa wingi, Oktoba 29,2025 kukipigia kura Chama Cha Mapinduzi,"amesema.

Pia amesema kwamba ataendelea kuwa pamoja na mgombea huyo na ikiwa atakuwa diwani atamuongoza ili kuhakikisha viporo vya miradi ya maendeleo vilivyobaki katika uongozi wake vinakamilika.









No comments:

Post a Comment