Hamisi Ramadhani 'H Baba': - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, February 9, 2012

Hamisi Ramadhani 'H Baba':

-Mkali wa Bolingo Fleva, anayetamani kufika Kimataifa
-Pia ajikita kwenye filamu sanjari na mchumba wake

Na Hamisi Magendela
WASWAHILI husema 'mchanganya mawili moja humponyoka' ni usemi unaotumiwa na jamii kuwataadharisha jamii kutoshirikisha masuala mawili kwa wakati mmoja kwani kuna
uwezekano mkubwa kutofanikiwa yote.

'Ni sawa na kusema 'mtaka yote hukosa yote', lakini nadiriki kusema msemo huo umekuwa tofauti kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Hamisi Ramadhani 'H Baba' kutokana na kufanya
mambo mawili kwa ufanisi mkubwa bila ya kuharibu sehemu
mojawapo.

H Baba, ambaye ni aliyezaliwa jijini Mwanza mwaka 1987, anasema alianza kushiriki katika sanaa hasa ya maigizo akiwa angali mdogo na kipaji kuanza kuonekana na wengi kutabiri
kuwa mafanikio makubwa mbeleni.

Msanii huyo aliyezaliwa pekee kwa wazazi wake, anasema kipaji chake kilianza kuoneka akiwa mdogo na kukiendeleza akiwa shule ya msingi Mbugani iliyopo Wilaya ya Nyamagana.
Anasema baada ya kuhitimu elimu ya msingi mwaka 1999,

Alijunga na shule ya sekondari Pamba na kuhitimu mwaka 2003 akiwa bado na kiu ya kuwa msanii wa kimataifa.Anaweka wazi kuwa kutokana na kujaliwa kuwa na vipaji vingi, baada ya kuhitimu kidato cha nne aliweza kuichezea vyema timu ya Pamba "Wanakawekamo" kabla ya kusaini kujiunga na Toto
Afrika ya Mwanza.

Anabaisha baada ya kuisaini kuichezea Toto Afrika, hakuweza kuitumikia timu kutokana na mapenzi yake kuwa katika sanaa ya maigizo pamoja na uimbaji.


Msanii H. Baba akiwa katika pozi
 Msanii huyo baada ya kuchukua kitita cha Toto alikwenda kurekodi kibao chake cha kwanza kinachoitwa  'Mpenzi Bubu' kilichotayarishwa na Said Comorien kwenye studio ya Metro.

Baada ya kurekodi kibao hicho mwaka 2004, na kufanya vizuri katika medani ya muziki wa kizazi kipya, alirudisha fedha za usajili kwenye uongozi wa timu hiyo na kuachana na mchezo wa
mpira wa miguu.

"Kutokana na mazoezi kuwa ni sehemu ya maisha yangu, huwa nafanya mazoezi mpira wa miguu kila siku katika viwanja wa Leaders Club ili kujiweka sawa kiafya," anasema H Baba.

Nyota huyo anasema baada ya kurudisha fedha hizo, alijipanga vyema kuhahakisha anafanya vizuri katika muziki huo chini ya meneja wake anaesimia kazi zake, Godsos Mkama.

Kupitia meneja wake huyo, aliachia wimbo mwingine mwaka 2006 uliofahamika kama Florida, Sophy na nyinginezo zilizotengenezwa katika studio ya Metro, na baada ya kipindi kifupi aliachia albamu iliyokuwa na nyimbo nane.

Albamu hiyo haikufanya vizuri kutokana na sababu mbalimbali, lakini ilimtangaza vyema katika tasnia hiyo ya muziki wa kizazi kipya na kila pembe ya Tanzania jina la H Baba likawa gumzo.

Baada ya kuachia albamu hiyo, ikafuatiwa na na nyingine kadhaa ikiwemo Poteza Poteza, ambayo ilifanya vizuri na kuzidi kumtangaza vyema kwenye tasnia hiyo.

Anasema kwa sasa akiwa katika maadalizi ya albamu ya pili, amebadilisha mtindo wa muziki wake na anatumia mtindo wa 'Bolingo Bolingo Fleva, ambao ni muunganiko wa muziki kutoka nchini Congo na Tanzania.

Albamu hiyo itakayokuwa na nyimbo nane, inatarajia kuingia sokoni Januari 2012, na itakuwa kwenye mtindo wa Bolingo Bolingo, na zimetayarishwa katika studio ya AM chini ya mtayarishaji Maneke.

H Baba anasema anavutiwa na msanii Mr Nice, kutokana na uhodari wake wa kuweza kuimba na kucheza, kitu ambacho kinamfurahisha sana.

"Msanii mzuri ni yule anayeweza kumudu mambo mengi kwa wakati mmoja bila kuharibu kingine, kwani ninapokuwa kwenye jukwaa napenda kulitawala zaidi kwa kucheza sanjari na kuimba
kwa pamoja, na ndicho anachokifanya Mr Nice," anasema H Baba.

Licha ya msanii huyo kuwa katika sanaa ya muziki, pia no muigizaji wa filamu, na kwa sasa tayari ametengeza kazi mbili akishirikiana vyema na mchumba wake anatayarajia kufunga
nae ndoa, Flora Mvungi.


Msanii Frola Mvungi
 "Nimezaliwa nikiwa msanii ndiyo maana namudu kwenye maeneo mengi ya sanaa, hivyo siwezi kuchanganya kazi kutokana na kuwa makini katika kuziandaa na kuzipa muda wa
kuzifanyia kazi na hiyo ndiyo siri ya mafanikio katika kazi zangu," anasema H Baba.

Anasema kati ya muvi hizo, tayari moja iko sokoni na inafanya vizuri katika mauzo na ya pili ambayo iko katika maandalizi ya mwisho ni 'Wema wa Mama wa Kambo' ambayo inatarajiwa
kwenda sokoni siku chache zijazo.

Msanii huyo ambaye anavutiwa pia na mwanamuziki Congo, Charles Kofii Antwaa Olomide, pamoja na kundi la Wenga BCBG, anasema ili wasanii waweze kufikia mafaniko ni vyema Serikali ikatilia mkazo suala la kudhibiti unyonyaji kazi za wasanii unaofanywa na wajanja kwa kudurufu kazi zao na kuwaacha wakiendelea kuwa masikini.

"Katika kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru, ni vyema Serikali ikatuangalia kwa jicho la huruma kutokana na kuibiwa kazi zetu na wafanyabishara wasiokuwa waaminifu ambao wanadurufu na
kujipatia kipato cha haramu kupitia kazi zetu," anahitimisha H. Baba, ambaye awali alikuwa na uhusiano na msanii mwingine wa filamu, Jackline Uwoya.

No comments:

Post a Comment