SHULE ZA KIMATAIFA ZATAKIWA KUTOA ELIMU KULINGANA NA MALENGO - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, April 23, 2026

SHULE ZA KIMATAIFA ZATAKIWA KUTOA ELIMU KULINGANA NA MALENGO


NA MWANDISHI WETU, KIBAHA


WAMILIKI wa shule za Kimataifa nchini wametakiwa kuboresha utoaji elimu kulingana na malengo yaliyowekwa ya fursa kwa watu wote kupata elimu.


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Elimu ya Ualimu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Mathias Mvula akimwakilisha Naibu Waziri wa Elimu Wanu Ameir wakati akifungua mafunzo ya wadau wa Shule za Kimataifa nchini kwenye Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha.


Mvula amesema kuwa uboreshaji wa sekta ya elimu una lengo la kuhakikisha wadau wa elimu wanatoa elimu bora na yenye viwango bora na vya kimataifa.


Naye Hassan Masawe kutoka Tanzania School Leadership Institute (TSLI) amesema kuwa mafunzo hayo yana lengo la kuboresha elimu inayotolewa na shule hizo kuwa na ubora baina ya elimu ya nchini na ile ya nje ya nchi.


Kwa upande wake Calista Mungwe Mkurugenzi wa shule ya Renie International ya Jijini Dar es Salaam amesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kuboresha uendeshaji wa Shule zao.

No comments:

Post a Comment