DC TEMEKE ATAKA UCHUNGUZI ' SHOWROOM' KUBAINI UTAKATATISHAJI FEDHA DAWA ZA KULEVYA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, July 23, 2026

DC TEMEKE ATAKA UCHUNGUZI ' SHOWROOM' KUBAINI UTAKATATISHAJI FEDHA DAWA ZA KULEVYA


NA MAGENDELA HAMISI


MKUU wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda ametoa wito kwa vyombo vya Ulinzi na Usalama kufanya uchunguzi katika showroom za magari wilayani humo.


Amedai kwamba baadhi ya maeneo hayo yanauza magari ya kifahari tofauti na mazingira hali inayotia shaka inawezekana upo uwezekana kutakatishwa fedha zinazotokana na uuzwaji wa dawa za kulevya.


"Haiwezekani kuona magari ya kifahari yanauzwa kiburugwa tena yakiwa rukuki hivi ni kweli mtu anaweza kuja Temeke kununua magari hayo,? huu natoa wito Kwa vyombo vya Ulinzi kuzichunguza ili kubaini ukweli

Hakika zinaibua maswali kutokana na kuuza magari mengi ya kifahari katika maeneo yasiyoonekana kuwa na soko linalolingana na biashara hiyo,"amesema.

 Mapunda ameyasema hayo leo, Julai 23, 2026 katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es Salaam kwenye Tamasha la Kuwafikia na Kuhamasisha Jamii dhidi ya Dawa za liloanza kwa matembezi kuanzia Kwa Azizi Alli.


Aidha amewataka vijana kujiepusha na matumizi ya madawa ya kulevya akisema athari zake huanza taratibu na kuharibu maisha ya mtumiaji kwa muda mrefu kabla ya matokeo yake kuonekana wazi.

Akizungumza katika kampeni ya kupinga matumizi ya madawa ya kulevya, alisema madawa hayo ni hatari kwa sababu huwavuta vijana hatua kwa hatua hadi kufikia kiwango ambacho ni vigumu kuacha au kurejea katika maisha ya kawaida.


Alisema vita dhidi ya madawa ya kulevya inahitaji juhudi katika kukata njia za usambazaji, kuzuia biashara haramu na muhimu zaidi kupunguza idadi ya watumiaji, kwani pasipo kuwa na mahitaji biashara hiyo itakosa soko.

Pia aliwataka wazazi kuanza kuwapa watoto elimu kuhusu madhara ya madawa ya kulevya tangu wakiwa wadogo ili wajenge uwezo wa kufanya maamuzi sahihi wanapokua.

Pia aliwasihi vijana kutofuata mkumbo wa kujaribu kila jambo kwa kisingizio cha fasheni, akisisitiza kuwa matumizi ya madawa ya kulevya huanza kwa majaribio lakini baadaye hugeuka utegemezi unaoharibu afya na maisha.

Aidha, alikemea tabia ya baadhi ya watu kuonesha utajiri kupita kiasi kupitia mitandao ya kijamii kwa kupiga picha wakiwa na fedha nyingi na magari ya kifahari bila maelezo ya chanzo cha mali hizo, akisema hali hiyo huwavutia vijana kutafuta utajiri wa haraka kwa njia zisizo halali.

Alisema vyombo vya ulinzi na usalama vinapaswa kuchunguza kwa kina vyanzo vya utajiri usioelezeka pamoja na biashara zinazoweza kutumika kutakatisha fedha zinazotokana na biashara ya madawa ya kulevya.

Amesisitiza kuwa, baadhi ya vijana wanaojihusisha na usafirishaji na biashara ya madawa ya kulevya wamekiri kushawishiwa na maisha ya kifahari ya wenzao waliodhani wamefanikiwa kwa njia rahisi, jambo linaloonyesha umuhimu wa kuendelea kutoa elimu kwa jamii.

Alitoa wito kwa wananchi kushirikiana na mamlaka kwa kutoa taarifa za wauzaji na wasambazaji wa madawa ya kulevya waliopo katika maeneo yao, akisisitiza kuwa ushindi dhidi ya biashara hiyo utapatikana pale jamii itakapokataa madawa ya kulevya kwa vitendo na si kwa maneno pekee.






No comments:

Post a Comment