CHALAMILA ATAKA TAFITI IFANYWE KUONDOA 'ZERO' KIDATO CHA NNE WILAYANI TEMEKE - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Monday, February 10, 2025

CHALAMILA ATAKA TAFITI IFANYWE KUONDOA 'ZERO' KIDATO CHA NNE WILAYANI TEMEKE


NA MWANDISHI WETU

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amewataka walimu wa Shule ya Sekondari wilayani Temeke na Wenyeviti Bodi husika kufanya tafiti ya kina ili kubaini sababu tofauti na zinazosemwa kwa lengo la kuondoa sufuri katika matokeo ya kidato cha nne.

Kiongozi huyo wa Mkoa wa Dar es Salaam, amesema kuwa hana tatizo na baadhi ya sababu zinazosemwa kuchangia wanafunzi kupata sifuri katika matokeo ya kidato cha nne ikiwemo utoro, uchelewaji kufika shule, kuishi mbali na shule, wengi kutojua kingereza na nyinginezo.

"Walimu Wakuu wa shule na Wadau wa elimu wametoa sababu kadhaa ambazo wanadhani zinachangia wanafunzi kupata four na zero, sasa nawataka kufanya tafiti zaidi ili kuja suluhu ya kuondoa sifuri," amesema


Chalamila amezungumza hayo, leo Februari 10, 2025 wakati akizungumza na Walimu Wakuu wa Sekondari na Wenyeviti wa Bodi wa Shule za Sekondari wilayani Temeke, katika siku ya kwanza kati ya tatu ya ziara yake.

Pia amewataka wakuu wa shule hizo na wenyeviti wa bodi wilayani humo wasiogope kufanya maamuzi yanayozingatia sheria kwa mujibu wa miongozo yao kwa ajili ya kuleta ufanisi katika sekta hiyo.

Tofauti na hayo pia amewataka kutafsiri miradi ya maendeleo hususani ya ujenzi wa miundombinu ya elimu ambayo imefanywa na Rais Samia Suluhu Hassan ili jamii ione kuwa umuhimu wa kutumia fursa hiyo jambo litakalosaidia kuinua ufaulu.

"Rais Samia amejenga shule za Sekondari na vyuo sasa wazazi wanatumiaje fursa hiyo, je wapo wanaojiuliza kwamba vijana wao wapo katika shule na vyuo hivyo,? naamini wazazi wakitimia fursa hiyo matokeo sifuri na four zitaondoka na kubaki daraja la kwanza, pili na tatu," amesema.

 Pia ametoa maelekezo kwa walimu hao na bodi , kukaa na wazazi na wadau wengine wa elimu ili kujadili kwa pamoja na kuimarisha ushirikishwaji wa wazazi kwenye masuala ya elimu.

Naye Mkuu wa wilaya ya Temeke,  Sixtus Mapunda amesema wanakwenda kujielekeza kwenye kutafuta chanzo cha changamoto ya wanafunzi kutofanya vizuri kwenye mitihani yao ili kupata suluhisho la kudumu kwenye elimu na kwamba pamoja na kuendelea kuimarisha miundombinu watashirikisha wazazi na wahitimu wa vyuo vikuu kwenye kada ya elimu.

Pia amesema Serikali, imetenga billion sita kwa ajili kujenga shule nyingine katika wilayani humo na kukarabati baadhi majengo ya shule.

MKUU huyo wa Wilaya ya Temeke, pia amesema kwamba kwa sasa wanatarajia kuajili walimu 200 wa masomo ya hesabu na sayansi.

Pamoja na hayo mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke Abdallah Mtinika ametaja changamoto ya lugha ya kingereza kama kikwazo cha ufaulu kwa wanafunzi huku Ofisa elimu Mkoa wa Dar es salaam, Gift Kyando akizungumzia changamoto ya usafiri kwa wanafunzi wanaosoma shule za mbali ambao wamekua wakiachwa vituoni na magari

No comments:

Post a Comment