
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Mwalimu Alexius Kagunze, atakuwepo kwenye kongamano hilo.
Na Dotto Mwaibale, Shinyanga
WAKAZI wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga pamoja na mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Alexius Kagunze wanatarajia kupata mambo mazuri kwenye kongamano maalumu la Upendo na Amani litakalofanyika Februari 28, 2026 mjini humo.
Kongamano hilo limeandaliwa na Umoja wa Wanamuzi Tanzania (TAMUFO).
Akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu kongamano hilo, Katibu Mkuu wa TAMUFO Stella Joel amesema maandalizi yote yamekamilika kwa asilimia 90 na kuwa vitu vilivyobakia ni vichache.
“Maandalizi ya kogamano yamekamilika ikiwa ni pamoja na wageni mbalimbali tuliowaalika kutoka ndani na nje ya nchi na wamethibitisha kushiriki,” alisema Joel.
Joel amewataja wageni watakaohudhuria katika kongamano hilo kuwa ni Dr. Khamis K. Said kutoka Tume ya Taifa ya UNESCO,ambaye atakuwa mgeni wa heshima ambapo wageni maalumu ni Profesa Kennedy Songwe kutoka Zambia na Mess Chengula Balozi wa Amani.
Amewataja wageni wengine kuwa ni Ambassador Dr. Frank Richard, Stella Joel, Dr. Christina Ngereza na Dr. Barwani.
Joel amewataja wageni wengine wataoshiriki ni Edelfrida Tibaija, Nesta Sanga, Emmanuel Mabisa na Baba Paroko Makassy Junior.
Joel alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha wana Shinyanga
kwenye kongamano hilo litakalofanyika Ukumbi wa Level One kuanzia Saa 6: 00 mchana
na kuendelea na kueleza kuwa waimbaji binafsi na kwaya mbalimbali zitakuwepo
kutoa burudani.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanamuzi Tanzania (TAMUFO), Ambassador Stella Joel
Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Nesta Sanga.
Mwimbaji wa nyimbo za injili, Emmanuel Mabisa.

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na. Usimamizi wa. Rasilimali Watu, Tume ya Taifa ya UNESCO Tanzania, Edelfrida. Stephen. Tibaija.








No comments:
Post a Comment