AFE KIPA AFE BEKI, UJENZI WA BARABARA ZA NGORONGORO HATUNA BREKI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, February 25, 2026

AFE KIPA AFE BEKI, UJENZI WA BARABARA ZA NGORONGORO HATUNA BREKI


NA MWANDISHI WETU

HAKUNA kulala, ndivyo kauli ya Kamishna wa Uhifadhi Ngorongoro ,Abdul-Razaq Badru baada ya kufanya ziara ya kukagua ukarabati wa barabara ndani ya hifadhi ”tutaendelea kuimarisha miundombinu yetu ya barabara yenye mtandao wa Km 646 ndani ya hifadhi kuhakikisha huduma inakuwa bora kwa watalii, wawekezaji na wananchi”


Akiwa kijiji cha Endulen Kamishna Badru amesema barabara zote kuanzia geti la Loduare hadi Golini yenye km 88, View Point hadi Naiyobi yenye Km 76, Kimba, Edulen hadi makao yenye Km 77 inayosimamiwa na TANROADS, Endulen hadi Ndutu yenye km 52, Ndutu - Golini yenye km 23, Makumbusho Olduvai kwenda Nasera yenye Km 54  na Barabara za kreta ya Ngorongoro zenye urefu wa Km 110  zitaendelea kuimarishwa na kupitika wakati wote


“Tunataka viwango vya utoaji huduma kwa wateja wetu viwe  juu,ndio maana mda wote tupo site kuhakikisha mitambo inafanya kazi na kila barabara inapitika mda wote wa majira ya mwaka" amesisitiza Kamishna Badru




No comments:

Post a Comment