NA MWANDISHI WETU
JAMII imetakiwa kutumia fursa ya Chuo cha Cha Ufundi Furahika kinachotoa elimu Bure kwa vijana ambao wameshindwa kujiendeleza kimasomo kutokana na changamoto mbalimbali.
Hayo yamebainishwa jana na Kaimu Kamisha Msaidizi, Faithmarry Lukindo kwa niaba ya Kamishna Mkuu Ustawi wa Jamii, katika mahafali ya Chuo hicho yaliyofanyika Ilala jijini Dar es Salaam ambapo wanafunzi wa kozi fupi katika fani za hoteli, umeme, udereva, ushonaji, Air Tikets, Bandari wahitimu mafunzo yao.
"Chuo hiki pia kinashirikiana na Ustawi wa Jamii, hivyo ni vema watoto wanaopatikana kuwa na changamoto kupitia ustawi wa Jamii wakawaleta katika chuo hiki ili wajiendeleze kielimu kupitia Mafunzo ya Amali yatakayowasaidia kuachana na utegemezi na kujikomboa kimaisha, amesema.
Ameongeza kuwa watoto wanapita katika mazingira magumu wakiachwa bila kusaidiwa wanatumbukia katika tabia hatarishi na kuwa mzigo kwa taifa kwa kupoteza nguvu kazi ya taifa.
Hakusita kuupongeza uongozi wa Chuo hicho kwa kutoa elimu ya Amali Bure na kuwa msaada tosha kwa vijana ambao wamepoteza matumaini kwa kukosa elimu itakayokuwa mtaji katika kujitafutia maisha ya kila siku.
"Pia niwatake wahitimu wakawe mabalozi wazuri huko wanapokwenda kuhitumikia jamii katika sekta mbalimbali na wakitangaze chuo kwa vijana wengine ili nao waje kupata elimu bure na wasikae vijiweni bila sababu ya msingi," amesema.
Aidha alitoa wito kwa maofisa Ustawi wa Jamii, wawe kipaumbele kuwaibua watoto wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi kwenye na kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha watoto hao wanapata fursa sawa na wengine katika kipata elimu, ujuzi na maarifa kwa maana Serikali imeweka mifumo thabiti kuhakikisha watoto wa rika zote na makundi yote wanapata huduma sawa.
Naye Mkuu wa Chuo hicho, Dkt David Msuya, amesema lengo la kutoa mafunzo ya Amali Bure ni kuunga mkono jitihada za Serikali ya Jamhuri ya Muungano inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Zanzibar inayoongozwa na Dkt Hussein Alli Mwinyi katika kuwaletea watanzania maendeleo.
Nafahamu Dkt Samia na Dkt Hussein wamefanya kazi kubwa kuwaletea watanzania, hivyo hatuna budi kuwaunga mkono ili kwa pamoja tuwawezeshe vijana kufikia ndoto zao kupitia elimu kwa wale waliokosa fursa ya kujienndelea kielemu na wanafunzi wanapifika chuoni kwetu wanacholipia na mtihani wa mwisho sh. 50,000 na fomu ya kujiunga 10,000.
"Sisi tunakusanya vijana wanaishi katika kaya maskini na kuwapa mafunzo ya amali bure ili vijana hao wafikie ndoto zao kwani tukiwaacha huko mtaani wanaweza kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya, kujiuza au kufanya vitu visivyo na maadili ndani ya nchi, amesema.
Pia muhitimu wa kozi ya Bandari, Nasra Abdalla, amesema anajuvunia kumalizo masomo hayo na sasa anakwenda kutimiza ndoto zake maisha katika mapambano ya ajira na akatoa wito kwa wenye uhitaji wa elimu kwenda katika chuo hicho kuchukua ujuzi Bure.
"Nashukuru uongozi wa Chuo na Serikali yetu chini, Dkt Samia kwa kufanikisha kutoa elimu Bure kwa vijana waliokosa fursa ya kuendelea na elimu kutokana na changamoto mbalimbali, nilikuja chuo hapa nikiwa sijui chochote na sasa naondoka nikiwa na ujuzi, nawashukuru sana," amesema.
No comments:
Post a Comment