TAWA YAKABIDHI MADAWATI 150 SHULE ZA MSINGI BARIDI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, November 22, 2025

TAWA YAKABIDHI MADAWATI 150 SHULE ZA MSINGI BARIDI


NA BEATUS MAGANJA, BARIADI

SERIKALI kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA Kwa kushirikiana na Kampuni ya uwindaji wa kitalii ya Bushman Safari Trackers imekabidhi madawati 150 Kwa shule za msingi tano (5) zinazopakana na  Hifadhi ya Maswa  wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu.


Shule zilizonufaika na mgao huo wa madawati ni pamoja na Shule ya Msingi Mwauchumu ambayo imepata madawati 30, damidami 30, Halawa 30, Mwabalizi 30 na Shule ya Msingi Nyawani ambayo nayo imepata madawati 30.


Akizungumza katika hafla ya kukabidhi madawati hayo iliyofanyika Novemba 21, 2025  katika Kijiji cha Halawa Kaimu Kamanda wa Uhifadhi kutoka TAWA Kanda ya Ziwa Mark Chuwa alisema madawati hayo yametokana na mradi wa Uwekezaji Mahiri (SWICA) ambao TAWA iliingia mkataba na Kampuni ya Kitalii ya Bushman Safari Trackers Ltd, ambapo mojawapo ya vipengere vya mkataba huo ni pamoja na kuhakikisha jamii zinazozunguka maeneo ya Hifadhi yaliyo chini ya usimamizi wa TAWA zinanufaika na rasilimali wanyamapori zinazopatikana katika maeneo husika.


"Hii ni sehemu ya utekelezaji wa mkataba huo, na ni manufaa ya moja Kwa moja ambayo inaenda Kwa jamii inayozunguka eneo letu" alisema Mark Chuwa.


Aidha Kamanda Chuwa ametoa rai Kwa wananchi wote wa Kanda hiyo kuendelea kushirikiana na Serikali kupitia taasisi hiyo katika kulinda rasilimali wanyamapori sambamba na kuwafichua wahalifu wote wanaofanya shughuli haramu za ujangili ndani ya hifadhi.


Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya jamii katika kitalu cha Maswa Kaskazini, Afisa Uhifadhi - Kitengo cha Ujirani Mwema Lusato Masinde alisema katika kuhakikisha jamii inayozunguka hifadhi ya Maswa inanufaika na shughuli za uhifadhi TAWA iliunda Kamati ya uwezeshaji jamii inayohusisha wahifadhi kutoka TAWA, Mwekezaji, Halmashauri ya Wilaya na mwakilishi wa wananchi ikiwa na majukumu ya kupanga, kutekeleza na kufanya ufuatliaji wa miradi itokanayo na mapendekezo ya wananchi.


Masinde alisema Kamati hiyo ilibaini   kuwa kulikuwa na changamoto na uhitaji mkubwa wa madawati katika vijiji vyote sita na hivyo TAWA Kwa kushirikiana na Bushman Safari Trackers Ltd iliamua kutengeneza madawati 150 Kwa ajili ya Shule zilizopo katika vijiji husika.


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Simon Simalenga akipokea na kukabidhi madawati hayo Kwa Shule zilizonufaika, aliishukuru na kuipongeza TAWA Kwa kushirikiana na Kampuni ya Kitalii ya Bushman Safari Trackers Kwa kuunga mkono jitihada za Serikali za kutatua changamoto za wananchi hususani kuboresha sekta ya elimu kwa shule za Mkoa wa Simiyu.


Aidha aliwataka wananchi hao kuona umuhimu wa kuendelea kulinda rasilimali wanyamapori zilizopo katika maeneo yao kwani zimekuwa na manufaa makubwa ikiwemo kuleta maendeleo na kutatua changamoto zinazowakabili.


"Ndugu wananchi, wanadau hawa wameleta madawati haya ni kwasababu Mwenyezi Mungu alitujalia kupata wanyamapori, kama tusingekuwa na wanyamapori basi leo hii hili tukio la kukabidhiwa madawati 150 lisingekuwepo"


"Niwapongeze sana TAWA na Mwekezaji Kampuni ya Bushman Kwa kuunga mkono juhudi za Serikali za kuboresha elimu nchini, niwaombe wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kulinda hifadhi zetu" alisema Mhe. Simalenga.


Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Halawa Boje Kalani aliwashukuru TAWA Kwa kuwapunguzia wananchi mzigo wa kuchangia Kwa  ajili ya kutatua changamoto ya ukosefu wa madawati kwenye shule yao ambapo alisema  kila mwananchi angepaswa kuchangia shillingi 12,000/= jambo ambalo huwashinda wengi.


Vilevile Meneja wa Mradi wa Uwekezaji Mahiri (SWICA) Rubani Willness Minja ameipongeza Serikali  Kwa kuwashirikisha wawekezaji wazawa katika mkataba wa SWICA unaolenga kuimarisha uhifadhi, kuwanufaisha wananchi na kuongeza mapato zaidi kwa Serikali.





1 comment:

  1. Kwa karibu mwaka mmoja, mume wangu aliniacha mimi na watoto wetu wawili. Aliacha kujali, akaacha kupiga simu, na akaondoka kabisa. Nilikuwa nimevunjika moyo, nimechanganyikiwa, na karibu kupoteza tumaini. Kisha siku moja, rafiki yangu aliniambia kuhusu Dkt. Dawn, mtu wa kiroho aliyepewa kipawa na ulimwengu ili kuwasaidia watu kurejesha upendo na amani.

    Mwanzoni, nilikuwa na shaka, lakini kitu kuhusu maneno yake kilinipa amani. Aliniambia haswa kilichokuwa kibaya na kwamba mtu alikuwa ametupa uchawi mkali kututenganisha. Aliandaa kazi maalum ya kiroho na uchawi wa kuungana tena kwa ajili yangu - na ndani ya siku chache, mume wangu alinipigia simu ghafla, akilia na kuomba msamaha.

    Tangu wakati huo, maisha yangu hayajawahi kuwa sawa. Ndoa yetu sasa ni tamu na yenye furaha zaidi duniani. Tunapendana zaidi kuliko hapo awali, na nyumba yetu imejaa vicheko na baraka.

    Lakini sio hivyo tu - Dkt. Dawn pia alisaidia kuondoa bahati mbaya na nishati hasi iliyozunguka familia yetu. Tangu wakati huo, kila kitu kimekuwa laini: amani nyumbani kwetu, maendeleo ya kifedha, afya njema, na furaha safi.

    Ninashukuru ulimwengu kila siku kwa kuniongoza kwa Dkt. Dawn. Kwa kweli ni mtu mwenye nguvu na mwanga wa kimungu. Ikiwa unapitia hali yoyote - huzuni, bahati mbaya, au kuchanganyikiwa - usikate tamaa. Mfikie na uache ulimwengu ufanye kazi kupitia yeye ili kubadilisha hadithi yako, kama vile alivyobadilisha yangu.

    Wasiliana naye kwenye WhatsApp: +2349046229159

    dawnacuna314@gmail.com

    ReplyDelete