TIMU YA WANAWAKE NGORONGORO YAKAA MGUU SAWA MASHINDANO YA SHUMMUTA MOROGORO - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, November 26, 2025

TIMU YA WANAWAKE NGORONGORO YAKAA MGUU SAWA MASHINDANO YA SHUMMUTA MOROGORO


NA MWANDISHI WETU 

Timu ya mpira wa Netiboli na mpira wa wavu ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imewasili mkoani Morogoro tarehe 25 Novemba 2025, imeendelea na program ya mazoezi katika viwanja vya Bwalo la JKT ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mashindano ya SHIMMUTA ambayo  yameanza tarehe 25 Novemba, 2025.


Akizungumza wakati wa mazoezi kwa ajili ya mashindano hayo yanayohusisha timu za mashirika mbalimbali, kocha wa timu ya Ngorongoro, Mathias Evarist ameeleza kuwa wachezaji wako tayari kuonyesha uwezo wao na kupambana katika michezo iliyoanza tarehe 25 Novemba hadi 06 Desemba 2025.


Kwa mujibu wa Afisa Michezo Mwandamizi wa NCAA, Yotham Gitige, katika mashindano hayo Ngorongoro inashiriki michezo ya mpira wa Netiboli, Mpira wa wavu na mchezo wa Riadha.







No comments:

Post a Comment