NA MWANDISHI WETU
UMOJA wa Wajasiriamali wa Mkoa wa Dar es Salaam umetoa wito kwa Watanzania kujiepusha na vurugu vinavyoweza kuhatarisha amani, utulivu wa taifa pamoja na uharibifu wa miundombinu.
Pia wamesisitiza kuwa vurugu haziwezi kuleta suluhu katika kudai haki na badala yake usababisha hasara hivyo wanalaani kwa nguvu zote baadhi wanasiasa, viongozi wa dini wanaoharibu amani ya nchi Kwa maslahi yao binafsi.
Wakizungumza leo Disemba 24 jijini Dar es Salaam na Waandishi wa Habari, wamesema unapinga vikali wito wowote wa uchochezi unaotolewa na wanaharakati wa ndani au nje ya nchi kwa maslahi binafsi kwani vitendo hivyo ulitumbukiza taifa kwenye hofu, hasara za kiuchumi.
Mjasiriamali wa Manispaa ya Ubungo Hussein Banze, amesema kuwa vurugu zilizotokea Oktoba 30 mwaka huu waathirika wakubwa ni wao Kwa maana walishindwa kufanya shughuli za kujiinguzia kipato huku Kundi lingine likipoteza ajira kutokana na miundombinu kuharibiwa.
Hivyo wamefuatilia kwa karibu matukio ya vurugu hizo na kubaini kuwepo kwa watu waliokuwa nyuma ya pazia wakihamasisha vitendo hivyo.
Pia vurugu hizo matukio zimeacha funzo kubwa kwa jamii kuwa uvunjifu wa amani hauwezi kuleta maendeleo.
Pia mjasiriamali wa Temeke, Lucy Peter amesema matukio ya Oktoba 29 yametosha kuwa somo." Tumeshuhudia athari zake na tumejifunza kuwa vurugu hazileti maendeleo wala suluhu ya amani,” amesema.
Pia Bakari Sufiani amesema amewasihi vijana wa Kitanzania, hususan wa kizazi cha Gen Z, kutowasikiliza watu wanaohamasisha vurugu, wakiwemo baadhi ya viongozi wa ndani, wanasiasa na wanamitandao wanaodaiwa kutumia mazingira hayo kwa maslahi binafsi au kisiasa.
Alisema waathirika wakubwa wa vurugu za Oktoba 29 walikuwa ni wafanyabiashara na wajasiriamali wadogo, waliopata hasara kubwa kutokana na uharibifu wa mali na kusimama kwa shughuli za kiuchumi.
“Tutaendelea kupaza sauti kupinga uchochezi. Tutapinga wanaharakati wanaojificha nje ya nchi kuhamasisha vurugu na maandamano, tutawakemea wanamitandao wanaoeneza chuki, wanasiasa wanaochochea vurugu na hata viongozi wa dini wanaochanganya siasa na majukwaa ya kiimani,” limeeleza tamko hilo.
Naye, Mzee Omary Suleiman, mfanyabiashara wa Soko la Kinondoni, amesema vurugu hizo zilitokana na uchochezi wa makusudi na kusisitiza kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kuhakikisha matukio kama hayo hayajirudii.
“Tanzania ni mimi, na mimi ni nchi. Tunaomba Watanzania wote waunge mkono jitihada hizi ili Tanzania ibaki salama, yenye amani na utulivu,” alisema.







No comments:
Post a Comment