MWANDISHI WETU
MIUNDOMBINU mbalimbali ya Kata ya Kijitonyama ambayo imo katika Halmashauri ya Kinondoni jijini Dar es Salaam inatarajiwa kufanyiwa marekenisho na kujenga upya ili kuondoa kero na kuwaleta maendeleo wananchi.
Diwani wa Kata hiyo ambaye pia ni Naibu Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Amani Baranda, amesema hayo leo, Feb 24 wakati akizungumza na Mwandishi wetu.
Amefafanua kwamba moundombinu inakwenda kufanyiwa kazi ni pamoja ujenzi wa Mto Kijitonyama ambao umekuwa kero hususani kipindi cha mvua za masika kutokana na kushindwa kuhimili maji na kusabisha mafuriko.
"Hali ya mafuriko kwa wananchi wanaoishi pembezoni mwa Mto Kijitonyama imekuwa kero na Sasa tunaraji kuusafisha Jambo litakalosaidia katika mvua hizo zinaokuja uweze kupitisha maji vizuri na baada ya hapo ujenzi utaanza rasmi", amesema.
Pia ameongeza kuwa wanakwenda.kijenga Ofisa ya Kata itayokuwa ya ghorofa moja baada ya awali kuchomwa moto katika vurugu zilizotokea kipindi cha Oktoba 29 mwaka Jana.
Miundombinu mingine ambayo inakwenda kutekelezwa ni ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami yenye urefu wa Km 0.4 kutoka wa Mtaa wa Ponta hadi Shule ya Sekondari, Salma Kikwete.
Aidha ameweka wazi kuwa mchakato wa ujenzi wa barabara hiyo unakwenda pamoja na kumalizia barabara nyingine za Mitaa ya Kijitonyama ambayo zinaendelea na ujenzi ikiwemo ya kwa Mchungaji, Kimario.
Kwa upande wa elimu, Diwani Baranda, amesema kwamba katika kata hiyo, Wana Shule mbili za Sekondari ambayo Kijitonyama ambayo Kijitonyama na Salma Kikwete ambayo imekuwa ikifanya vibaya katika matokeo ya kidato cha nne na sasa wanakwenda kutafuta mwarobaini wake.
Kutokana na kufanya vibaya kwa Shule ya Sekondari ya Salma Kikwete, tumekaa na walimu na wazazi, tumebaini changamoto kadhaa ambazo tunaenda kuzifanyia kazi, ikiwemo utoro na makuzi.
Hivyo Kwa sasa tumeamua katika kikao hicho kwamba kutakuwa na mitihani ya kujipima kila wiki na kila mwezi tutakuwa na kikao cha tathimini ya matokeo na ufundishaji kupata njia ya pamoja ya kuinua ufaulu, kwani Kwa sasa shule ina zero 94 Kwa matokeo ya kidato cha nne.





No comments:
Post a Comment