BENKI YA VIJANA KUWEZESHA BUNIFU, VIJANA KUNUFAIKA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, April 22, 2026

BENKI YA VIJANA KUWEZESHA BUNIFU, VIJANA KUNUFAIKA


NA MWANDISHI WETU


KUFUATIA kuanzishwa benki ya vijana watanufaika kupitia bunifu zao mbalimbali zitokanazo na mitandao ya kijamii.


Akizungumza na waandishi wa habari Kibaha kuhusu bajeti iliyowasilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana Dk Joel Nanauka Jijini Dodoma, Dk Ivan Rutatin amesema benki hiyo itakuwa mkombozi kwa vijana.


Rutatina amesema kuwa vijana walikuwa wakipata changamoto kubwa ya kupata fedha kwa ajili ya kuendesha shughuli zao za bunifu.


"Kupitia benki hiyo vijana watapata mitaji watanufaika mbali ya kupitia bunifu zao pia wataweza kuanzisha viwanda vidogo na kujiajiri na kuajiri wenzao,"amesema Rutatina.


Aidha amesema kuwa viwanda hivyo vitasaidia kuondoa changamoto ya ajira kwa vijana ambao walikuwa wakipata changamoto kubwa ya kukosa mitaji.



No comments:

Post a Comment