IZO BETRI ZAZINDULIWA DAR, HAZITUMII MAJI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, May 12, 2026

IZO BETRI ZAZINDULIWA DAR, HAZITUMII MAJI


NA MWANDISHI WETU

KAMPUNI ya Izo Mottors Company Ltd, imezindua betri mpya za magari ambazo zinatarajiwa kusambazwa mikoani siku chache zijazo.


Akizungumza leo na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Izo Mahenge amesema kwamba betri hizo zina ubora wa hali ya juu na hazitumii maji na badala  yake inatumia drayer.


"Betri zetu zina ubora wa hali ya juu na zinatumika katika magari ya aina tofauti na zinapatiikana kwa bei nafuu na zinatengenezwa hapa Tanzania," amesema.

 

Licha ya uzinduzi huo, pia kampuni hiyo, imeingia makubaliano ya ushirikiano ya kibiashara na msanii Dotto Magari ambaye amekuwa balozi wa kutangaza betri hizo.


Ameongeza kuwa kwa Sasa betri hizo zinapatiikana Mtaa Narungombe Kariokoo jijini Dar es Salaam na kuwaomba wadau kujitokeza kuwa Mawakala wa kampuni hiyo ya Kitanzania.

No comments:

Post a Comment