WAZALISHAJI 20 KILIMO IKOLOJIA WAPEWA MAFUNZO - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, June 25, 2026

WAZALISHAJI 20 KILIMO IKOLOJIA WAPEWA MAFUNZO

NA MWANDISHI WETU

WAZALISHAJI 20 wa mazao ya kilimo ikolojia kutoka mikoa ya Arusha na Kilimanjaro wamejifunza teknolojia  kuongeza thamani ya mazao.


Teknolojia hiyo wamejifunza mkoani Morogoro walipotembelea Kiwanda cha Intermech, kinachojihusisha na utengenezaji wa mashine mbalimbali za uchakataji wa mazao.


Ziara hiyo ya mafunzo imeratibiwa na Shirika la Island if Peace (IDP) na Mtandao wa Vikundi vya Wakulima mkoani Arusha (MVIWAARUSHA), chini ya Mradi wa ECO FOOD.


Wajasiriamali hao wamesema teknolojia ya kuongeza thamani mazao inayotelezwa kiwandani hapo imewapa moyo wa kuendeleza kilimo ikolojia.


"Kupitia ziara hii, washiriki walijifunza namna mashine zinavyoweza kusaidia kupunguza upotevu wa mazao baada ya mavuno, kuongeza ubora wa bidhaa, kuboresha vifungashio, kuongeza muda wa kuhifadhi bidhaa na hatimaye kuongeza thamani pamoja na kipato cha mjasiriamali,".


Wamesema uwekezaji katika teknolojia za uchakataji si tu unaongeza thamani ya mazao, bali pia unafungua fursa za masoko, ajira na kuchangia katika kujenga mfumo wa chakula endelevu na wenye tija zaidi.


Mradi wa ECO-FOOD unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya IDP na MVIWAARUSHA, ukiwa na lengo la kuimarisha mifumo ya chakula endelevu kupitia kilimo ikolojia, kuongeza thamani ya mazao, na kuwawezesha wajasiriamali katika mnyororo mzima wa chakula. 


Kupitia ushirikiano huu, washiriki wanapata fursa za mafunzo, kubadilishana uzoefu na kujengewa uwezo ili kuchangia mabadiliko chanya katika uzalishaji, usindikaji na biashara za mazao ya kilimo ikolojia.




No comments:

Post a Comment