DCEA YAWANOA WAANDISHI KUHUSU KEMIKALI BASHIRIFU - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, July 3, 2026

DCEA YAWANOA WAANDISHI KUHUSU KEMIKALI BASHIRIFU


NA MWANDISHI WETU

WAANDISHI wa Habari jijini Dar es Salaam wamejengewa uwezo wa kuandika kwa usahihi kuhusu Kemikali Bashirifu ambayo imekuwa ikitumika kama mbadala wa dawa za kulevya Kwa lengo la kukwepa mkono wa sheria.


Katika semina hiyo ambayo imefanyika leo jijini humo, imeelezwa kuwa Kemikali Bashirifu si Dawa za Kulevya bali ni dawa tiba  zenye asili ya kulevya ambazo zinatumika kama tiba kwa binadamu na wanyama.


Kwamujibu wa Kamishina Msaidizi Uchunguzi wa mamlaka hiyo, Ziliwa Machibya amesema baadhi ya dawa hizo zinatumika kwa mtu anayefanyiwa upasuaji au mwenye maumivu makali.


"Dawa hizo mara nyingi utumika kutuliza maumivu, mawazo, hivyo ikitumiwa pasipo utaratibu au ushauri wa daktari muhusika anaweza akaingia kwenye uraibu.


Hivyo zisipodhibitiwa matumizi yake zinaweza kuwa janga kwa jamii zikiwa zinatumika kiholela, Kwa hiyo nguvu inajitajika kwa kushirikiana na wadau nanyi waandishi  ambao ni jeshi kubwa kuhakisha tunapambana na matumizi ya dawa hizo kama mbadala wa dawa za kulevya," amesema.


Ameongeza kwamba dawa hizonzimekuwa zikitumika baada ya kudhibitiwa kwa uingizwaji wa dawa za kulevya na wengine wakaona hiyo ni njia mbadala kwani hazina utofati na dawa za kulevya.


Aidha amefafanua kwamba kutokana na kuwepo udhibiti mdogo kwenye baadhi ya hospitali na maduka ya dawa zinafanya ziingie mtaani na kuleta athari kwa watumiaji.



Aidha zipo  sheria zinazohusika na udhibiti wa kemikali bashirifu, kwa mtumiaji na mchepushaji anayetumia kutengenezea dawa za kulevya.


 Amefafa kuwa kemikali Bashirifu ni halali kwa matumizi yaliyosahihi ila zikichepishwa hapo ndipo tatizo linapoanza kwani utumika kutengeneza dawa za kulevya ambalo ni kinyume na sheria za nchi.


Aidha Kamshna Machibya amezitaja sheria  hizo ni Sheria ya kemikali za Viwandani na Majumbani (Udhibiti na Usimamizi) Na. 3 ya Mwaka 2003.


Nyingine ni Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Na. 5 yaMwaka 2015 (R.E 2020), Vifungu vya (14, 15, 15A) pamoja na Sheria ya Dawa na Vifaa Tiba Na. 1 ya Mwaka 2003 marekebisho ya Sheria ya Fedha 2019)


Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kudhibiti Usafirishaji haramu wa Dawa za Kulevya wa mwaka 1988.


Kutokana na sheria hizo pia ametaja kemikamili bashirifu zilizokamatwa maeneo mbalimbali duniani ni Acetone - lita 3360, Ethanol - lita 8750, Azobisisobutyronitrile - kilo 60, Hydrochloric Acid - kilo 1400, Lead acetate - kilo 5000, N-methylformamide-lita 1890.


Dawa nyingine ni Toluene lita 420, Tartaric acid kilo 375, (2-bromoethyl)benzene kilo 13.5, acetic acidi kilo 4.4, Acetone kilo 22.5, benzyl alcohol kilo 434, ethanol kilo 358, hydrochloric acid 1834.36, methylamine 202.5, tartaric acid kilo 21, toluene kilo 67.5


Akitoa mifano ya Uchepushwaji nchini amesema uchunguzi  ulibaini kiasi cha kilo 12 za kemikali bashirifu aina yapseudoephedrine zilikuwa zimechepushwa katika mchakato wa uzalishaji wa dawa za kikohozi na kupelekea uteketezaji wa lita10,000 za dawa zenye pungufu ya kiambata hai cha kemikali hiyo


Pia ukamatwaji wa tani 21.7 za acetic anhydride nchini Pakistani zilizosafirishwa kutoka Tanzania kwa jina bandia la acetic acid


“Mwaka 2025, jumla ya tani 31.76 na lita 183.500 zà kemikali bashirifu zilikamatwa hapa Nchini. Zimezuiliwa kemikali bashirifu tani 734 Kuingia nchini kinyume cha taratibu," amesema.


Amefafanua kuwa kiasi hicho kinahusisha tani 4 za kemikali bashirifu za kutengeneza dawa ya kulevya aina ya fentanaili(kilipangwa kusafirishwa kwenda Mexico kwa jina bandia la protein biotine) pamoja na kugundulika kwa maabara bubu ya kutengeneza methafetamine mpakani Namanga.







No comments:

Post a Comment