TAMISEMI, WORLD VISION, WAJADILI MKAKATI WA KUBORESHA USTAWI WA WATOTO - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, July 29, 2026

TAMISEMI, WORLD VISION, WAJADILI MKAKATI WA KUBORESHA USTAWI WA WATOTO


NA OWM – TAMISEMI, DODOMA


NAIBU Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI), Sospeter Mtwale, ameongoza kikao kazi kati ya ofisi yake na Shirika lisilo la Kiserikali la World Vision Tanzania, kilicholenga kujadili Mkakati wa Jubilee 2026–2030 uliowasilishwa na World Vision Tanzania wa kuboresha ustawi wa watoto nchini.


Mkakati huo  unalenga kuwafikia watoto moja kwa moja kupitia programu za afya, lishe, elimu, ulinzi wa mtoto, huduma za maji safi na usafi wa mazingira (WASH), pamoja na kuimarisha kipato cha kaya. 


Akifafanua kuhusu lengo la mkakati huo, leo Julai 29,2026 Jijini Dodoma Mkurugenzi wa Ubora na Mikakati wa World Vision Tanzania, Simon Moikan amesema, mpango huo  unakusudia kushughulikia changamoto tatu zinazoendelea kuathiri mamilioni ya watoto nchini ambazo ni utapiamlo, utoro wa shule na ukatili dhidi ya watoto.


Mara baada ya Mkakati huo kuwasilishwa, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu –TAMISEMI Bw. Sospeter Mtwale alitoa fursa kwa wataalamu kutoka idara mbalimbali za Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI zinazoshughulikia masuala ya ustawi wa watoto pamoja na wataalamu kutoka World Vision Tanzania, kujadiliana kuhusu namna bora ya kuratibu ushirikiano katika utekelezaji wa mkakati huo iwapo mamlaka itaridhia, pindi utakapowasilishwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI kwa hatua za uidhinishaji.


Majadiliano hayo   yanaakisi dhamira ya kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na wadau wa maendeleo katika kuhakikisha watoto wa Tanzania wanapata huduma bora na mazingira salama yanayowezesha ukuaji, maendeleo na ustawi wao.







No comments:

Post a Comment