WAKULIMA, WANANCHI WASHAURIWA KUPANDA MITI YA MATUNDA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, July 3, 2026

WAKULIMA, WANANCHI WASHAURIWA KUPANDA MITI YA MATUNDA


NA MWANDISHI WETU

WAKULIMA na wananchi kwa ujumla wameshauriwa kupanda miti ya matunda, migomba na viungo viliyofanyiwa utafiti kwa kuwa yana faida kwa afya za walaji na kiuchumi.


Ushauri huo umetolewa na  Mtafiti wa Taasisi ya Utafiti Tanzania (TARI) Tengeru Tengeru Emmanuel Pallangyo wakati akizungumza na mwandishi wa Raia Mwema Digital.


Amesema TARI inafanya utafiti wa mazao mbalimbali kama miti ya matunda, viungo au vikolezo na mahindi, mpunga na mengine, hivyo wanashauri wakulima kupanda mazao hayo kwa kuwa yana faida nyingi.


Pallangyo amesema mazao kama ndizi, matunda na viungo au vikolezo yanaweza kulimwa kwenye bustani za nyumbani, hivyo wanawaomba wananchi kutembelea Banda la TARI lililopo kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF), ili kujipatia mbegu bora zilizotafitiwa.


"Hapa sabasaba tuna mbegu za mchaichai, parachichi, pera, migomba, korosho na nyingine nyingi, njooni mfaidi taasisi yenu," amesema.


Mtafiti huyo amesema mbegu zote ambazo wanazalisha zinangatia utafiti, ili kuwezesha wananchi wa maeneo yote ya Tanzania kutumia.


"Tunahamasisha matumizi ya viungo kwenye vyakula au chai kwa sababu tiba na chakula kuwa na harufu nzuri," amesema.


Pallangyo amesema pamoja na TARI kuzalisha mbegu nyingi kitafiti, bado wakulima wanaamini kwenye mbegu zilizopitwa na wakati, hivyo kukosa tija kwenye uzalishaji.


Mkulima wa zao migomba kutoka Chalenzi wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, Martin  Mayengela amesema umevutiwa na mazao ya yanayozaliswa  TARI na ndio maana amenunua na kwenda kupanda.


"Mimi nimekuja hapa kununua miche ya migomba na parachichi nikapande shambani kwangu naamini itaenda kufanya vizuri," amesema.




No comments:

Post a Comment