WANAFUNZI 6,800 KUSHIRIKI FEASSA 2026 MOROGORO - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, August 11, 2026

WANAFUNZI 6,800 KUSHIRIKI FEASSA 2026 MOROGORO


NA OWM - TAMISEMI


Jumla ya wanafunzi 6,800 kutoka nchi tano za Jumuiya ya Afrika Mashariki wanatarajiwa kushiriki Mashindano ya Michezo ya Wanafunzi wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (FEASSA) 2026, yanayofanyika nchini Tanzania, mkoani Morogoro.


Hayo yamesemwa leo Agosti 11, 2026 na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mashindano hayo.


Amesema kuwa  kwa  mwaka huu, mashindano hayo yanatarajiwa kushirikisha wanafunzi takribani 6,800 kutoka nchi za Burundi, Kenya, Rwanda, Uganda na wenyeji Tanzania., ambapo  jumla ya wanafunzi 1,510 wanatoka Tanzania.


Amesema katika mashindano ya FEASSA 2026, jumla ya michezo 20 itashindaniwa na wanafunzi wa shule za sekondari, michezo sita kwa upande wa shule za msingi, pamoja na michezo minne kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.


Ameongeza kuwa, mashindano hayo yataanza rasmi Agosti 12, 2026, huku hafla ya ufunguzi rasmi ikitarajiwa kufanyika Agosti 16, 2026 ambapo Mgeni rasmi katika hafla hiyo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.







No comments:

Post a Comment