MZEE WARIOBA AANGUKA AKIHUTUBIA, AKIMBIZWA HOSPITALI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Monday, September 7, 2026

MZEE WARIOBA AANGUKA AKIHUTUBIA, AKIMBIZWA HOSPITALI


 NA MWANDISHI WETU

HABARI zilizotufikia hivi Punde zinasema Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba, ameanguka ghafla wakati akizungumza katika mkutano wa kitaifa wa kutafakari hali ya kisiasa nchini Tanzania.


Warioba alikuwa miongoni mwa wazungumzaji wakuu katika mkutano huo unaoandaliwa na Tanzania Centre for Democracy (TCD), ambapo alizungumzia masuala ya kisiasa na mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya.


Tukio hilo limetokea wakati akiendelea kuzungumza, Mzee Warioba alianguka ghafla, hali iliyosababisha shughuli za mkutano kusitishwa kwa muda.


Mwenyekiti wa TCD, Dorothy Semu, alitangaza mapumziko mafupi ili kutoa nafasi kwa hatua za kumsaidia Warioba kuchukuliwa, na baada ya takribani muda dakika chache, Warioba alisimama na kuondoka katika eneo la mkutano huo. 


Hata hivyo, Bado hakuna taarifa rasmi kuhusu hali yake kiafya kwa sasa endelea kutufuatilia Kwa taarifa zaidi


No comments:

Post a Comment