MAPATO YA STAMICO YAPAA KUTOKA SH BILIONI 1.3 HADI 149.8 - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, October 16, 2026

MAPATO YA STAMICO YAPAA KUTOKA SH BILIONI 1.3 HADI 149.8

 


Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeeleza kuimarika kwa mapato yake kutoka takribani Sh bilioni 1.3 hadi Sh bilioni 149.8, huku likiendelea kuweka mikakati ya kuongeza uzalishaji, kuimarisha miradi ya uchimbaji na kupanua huduma kwa wachimbaji wadogo nchini.

Katika kuimarisha shughuli zake, shirika hilo limeweka mikakati ya kuongeza mitambo ya uchorongaji, kuendeleza viwanda vya uchakataji wa madini na kuwaunganisha wachimbaji wadogo na taasisi za fedha ili kurahisisha upatikanaji wa mitaji.

Akizungumza na wahariri na waandishi wa habari katika kikao kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR), jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa STAMICO, Dkt. Venance Mwase, alisema shirika limebaini changamoto mbalimbali zinazowakabili wachimbaji wadogo, zikiwemo ukosefu wa taarifa za kijiolojia, mitaji, elimu ya uchimbaji na teknolojia bora.




No comments:

Post a Comment