NGORONGORO YACHANJA MBUGA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, October 31, 2026

NGORONGORO YACHANJA MBUGA


NA MWANDISHI WETU


Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro itaendelea kutumia vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi katika kutangaza vivutio vya utalii kitaifa na kimataiifa ili kuvutia watalii wengi zaidi.


Akitoa mada katika mkutano wa waandishi wa habari vijijini Afisa  Uhifadhi Mkuu Uhusiano kwa umma Ngorongoro, Kassim Nyaki amesema vyombo vya habari vina nguvu kubwa katika kufikia watu wengi kwa wakati mmoja hivyo Ngorongoro inatumia Fursa hiyo kuhakikisha kila Mtanzania anafikiwa.


Akitoa Mada katika mkutano huo Afisa Utalii Ngorongoro COII Hillary Kimaro ameeleza kuwa Ngorongoro ni  kitovu cha Maajabu mengi (Destination of Many Wonders) ambapo eneo hilo la Urithi  wa Dunia linalokusanya wanyamapori, malikale, urithi wa utamaduni pamoja na kushuhudia pumzi ya kwanza ya ndama kuzaliwa kabla ya kuhama kwa nyumbu katika eneo la Ndutu.


Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (RUJAT) Neville Meena ameipongeza Mamlaka ya  Hifadhi ya Ngorongoro kwa kuthamini mchango wa waandishi wa habari katika kutangaza utalii wa nchi yao ili kuendelea kuvuta maelfu ya watalii kutoka kila pembe ya dunia






No comments:

Post a Comment