"NGORONGORO, TANAPA DAM DAM" - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Sunday, November 15, 2026

"NGORONGORO, TANAPA DAM DAM"


NA MWANDISHI WETU 

(NCAA) imekabidhi Shirika la hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kituo cha mwitikio wa haraka kwa ajili ya kukabiliana na changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu kilichojengwa  katika kijiji cha Mwaseni, kata ya Mloka, Rufiji Mkoni Pwani.


Akizungumza wakati wa kukabidhi kituo hicho Naibu Kamishna wa Uhifadhi, utalii na maendeleo ya jamii Ngorongoro Joas Makwati , amesema ujenzi wa vituo vya askari wa wanyamapori  unalenga kutoa mwitikio wa haraka kwa matukio ya wanyamapori wakali na waharibifu katika hifadhi ya Nyerere kama sehemu ya mchango wa Ngorongoro  kuisaidia Serikali za kukabiliana na changamoto ya wanyamapori na kuimarisha usalama wa wananchi.


“Baada ya kukamilisha kituo hiki Serikali itahakikisha askari watakuwa karibu na wananchi na wataweza kuwahi kwa haraka pale wanyama wanapovamia makazi ya watu ili tuhakikishe wananchi wanakuwa salama na mali zao kama Ilani ya chama cha mapinduzi inavyotuelekeza ," amesema *Kamishna Makwati


Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwaseni, Hemed Rashid, ameishukuru Ngorongoro  kwa ujenzi wa kituo hicho na kuahidi watakilinda na kushirikiana na askari wa uhifadhi kukabiliana na wanyamapori waharibifu.


Kwa upande wake Mwakilishi wa Kamishna wa uhifadhi TANAPA, PCO Davis Mushi ameshukuru uongozi wa Ngorongoro na kueleza kuwa “kituo hicho cha mwitikio kitaongeza ufanisi wa kazi za askari  wa uhifadhi kuwa na ofisi, makazi bora na uwezo wa kulinda na kudhibiti wanyamapori wanaoleta uharibifu kwa wananchi wa Mloka na vijiji jirani."





No comments:

Post a Comment