'TABASAMU LA WAHARIRI NGORONGORO" - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Sunday, November 22, 2026

'TABASAMU LA WAHARIRI NGORONGORO"

 

Wahariri wa vyombo vya habari nchini kupitia *Jukwaa la wahariri* wamepigwa na tabasamu baada ya kutembelea *Hifadhi ya Ngorongoro* na kushuhudia maajabu yenye simulizi mnato.


Wakiongozwa na Mwenyekiti wa Jukwaa hilo *Deodatus Balile* wahariri hao walielezwa kuhusu uthibitisho wa kisayansi unaodhihirisha kuwa binadamu wa kale alipatikana katika *bonde la Olduvai*.


Maajabu mengine waliyopata simulizi yake ni *mchanga wa kunogesha mahaba* ama mchanga unaohama ambao pamoja na mambo mengine ni sehemu pekee ya kuimarisha upendo hasa *mahaba yaliyolegalega*.


Wahariri wa vyombo vya habari nchini kupitia Jukwaa la wahariri wamepigwa na tabasamu baada ya kutembelea Hifadhi ya Ngorongoro na kushuhudia maajabu yenye simulizi mnato.


Wakiongozwa na Mwenyekiti wa Jukwaa hilo *Deodatus Balile* wahariri hao walielezwa kuhusu uthibitisho wa kisayansi unsodhihirisha kuwa binadamu wa kale alipatikana katika *bonde la Olduvai*.


Maajabu mengine waliyopata simulizi yake ni *mchanga wa kunogesha mahaba ama mchanga unaohama* ambao pamoja na mambo mengine ni sehemu pekee ya kuimarisha upendo hasa mahaba yaliyolegalega.


Kamishna wa Uhifadhi, Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro *Dkt.Abdul-Razaq Badru* amewaeleza wahariri hao kuwa Hifadhi ya Ngorongoro ina mvuto mkubwa kutokana na uwezo wake wa vivutio na Urithi wa utamaduni.


Kamishna *Dkt. Badru*amewaeleza wahariri hao kuwa  katika kuelekea Mashindano ya *AFCON* mwaka 2027, *Ngorongoro* imejipanga kikamilifu kupokea wageni wakaokuja kutalii ambapo kwa sasa nguvu kubwa ni kuboresha miundombinu ya utalii kuimarisha mifumo ya malipo, ujenzi wa barabara kutoka geti la *Loduare hadi Seneto  km 29.5* kwa tabaka gumu sambamba na  kuimarisha kivutio cha maporomoko ya maji Endoro ambapo ujenzi wa ofisi za kisasa za kutolea huduma na njia za watembea kwa miguu zinajengwa katika eneo hilo.


Akiongea kwa niaba ya Wahariri, Mwenyekiti wa jukwaa wa Wahariri Deodatus Balile ameeleza kuwa Ngorongoro ni mdau muhimu katika kuchangia  pato la taifa na huduma za wananchi kupitia mapato ya utalii na  kusema kuwa jukwaa hilo litaendelea kushauri kwa karibu kuhusu hifadhi hiyo.


Kamishna wa Uhifadhi, Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro Dkt.Abdul-Razaq Badru amewaeleza wahariri hao kuwa Hifadhi ya Ngorongoro ina mvuto mkubwa kutokana na uwezo wake wa vivutio na Urithi wa utamaduni.


Kamishna Dkt. Badru amewaeleza wahariri hao kuwa  katika kuelekea Mashindano ya AFCON mwaka 2027, Ngorongoro imejipanga kikamilifu kupokea wageni wakaokuja kutalii ambapo kwa sasa nguvu kubwa ni kuboresha miundombinu ya utalii kuimarisha mifumo ya malipo, ujenzi wa barabara kutoka geti la Loduare hadi Seneto  km 29.5 kwa tabaka gumu sambamba na  kuimarisha kivutio cha maporomoko ya maji Endoro ambapo ujenzi wa ofisi za kisasa za kutolea huduma na njia za watembea kwa miguu zinajengwa katika eneo hilo.


Akiongea kwa niaba ya Wahariri, Mwenyekiti wa jukwaa wa Wahariri Deodatus Balile ameeleza kuwa Ngorongoro ni mdau muhimu katika kuchangia  pato la taifa na huduma za wananchi kupitia mapato ya utalii na  kusema kuwa jukwaa hilo litaendelea kushauri kwa karibu kuhusu hifadhi hiyo.







No comments:

Post a Comment